Facebook Comments Box

Friday, March 1, 2013

POLISI WANATUHUMIWA KUMPIGA RISASI MWALIMU HUYU


PictureMwalimu mmoja wa Shule ya Sekondari Kitulo wilayani Makete aliyefahamika kwa jina la Casto Sote Kawamba ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa Jeshi la Polisi, Makete

Mkuu wa polisi wa wilaya ya Makete, SP Peter Kaiza akizungumza na FrancisGodwin blog kuhusu tukio hilo lililotokea katika eneo la benki ya NMB tawi la Makete juzi majira ya saa moja na robo alisema  kuwa mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenki kupitia mashine ya  kutolea  pesa ya ATM akiwa na pikipiki, na kuamriwa na askari mmoja aitwaye Jose Msukuma, kuvaa kofia.

Inadaiwa  kuwa kisa cha mauwaji yake ni madai ya kutokuvaa kofia na baada ya kuitwa na askari hao alikaidi amri na kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa lindoni.

Hata  hivyo  mmoja kati ya  askari ambaye   jina lake halikufahamika mara  moja alisikika  akidai kuwa  chanzo cha mtu huyo kupigwa  risasi  ilikuwa akihisiwa  kuwa ni jambazi baada ya  kufika kwa usafiri wa pikipiki (bodaboda) na kuhisiwa kuwa amefika  kwa ajili ya kuora katika benki hiyo na hivyo askari katika hali ya  kujihami alimpiga risasi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete, Idd Nganya ambaye ndie mwajiri wa marehemu amesema kuwa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Makete wakati utaratibu wakusafirisha mwili huo kwenda kwao Mbeya kwa ajili ya mazishi ukiendelea.

Mganga mkuu mfawidhi ambaye ni msemaji wa hospitali ya wilaya ya makete Dr Michael Gulaka amesema kuwa wao walipokea mwili wa marehemu na sio majeruhi.
kwa habari zaidi na picha ingia FrancisGodwin blog


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU