Facebook Comments Box

Thursday, February 7, 2013

HII NDIO HALI MBAYA INAYO WAKABILI WATALII WALIOTAKA KUWEKA HISTORIA YA DUNIA MLIMA KILIMANJARO


???????????????????????????????
Picha ikionesha heliKopta  ikiwa inapeleka chakula na maji kwa waanga walioshindwa kushuka kwa kutumia miamvuli maalum katika mlima kilimanjaro
Marubani waliopanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuruka kutoka kileleni kwa kutumia miamvuli maalum wanaendelea kusota baada ya hali mbaya ya hewa kuwazuia kutekeleza azma yao.
Wakiwa wametimiza siku 11 sasa tangu waanze safari yao mlimani, inaripotiwa kuwa hivi sasa wameanza kuishiwa akiba ya chakula na helikopta iliyosheheni maji na shehena nyingine ya vyakula imeruka kwenda kileleni siku ya Jumatano ili kuvidondosha kwa wahanga hao.
Marubani hao zaidi ya 100 walikuwa wanatarajiwa kuruka kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro kwa kutumia miamvuli maalum (Paragliding)na kutua eneo la Kibosho siku ya Jumanne, lakini hadi leo hii (Alhamisi) bado wako mlimani.
Mkuu wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro Erastus Lufungulo amesema hali ya hewa mlimani hapo bado inaendelea kuchafuka kwa upepo mkali na mawingu mazito.
Marubani hao wa kimataifa, wanatoka nchi mbalimbali duniani, walitarajiwa kuwa binadamu wa kwanza kabisa kuruka kutoka kilele hicho kirefu zaidi barani Afrika.
Helikopta maalum ilitumwa mara kadhaa kuzunguka mlimani kwa siku mbili mfululizo ili kujaribu kuona marubani hao 100 wakiwemo wanawake 30 watakuwa wamefika wapi. Na siku ya jumanne usiku, watu 15 waliokuwa kwenye timu hiyo walirudishwa chini na kukimbizwa hospitali baada ya kuugua.
“Ni kweli zoezi limeshindikana hadi sasa ila hatuna wasiwasi na usalama wa watalii hao kwani tumekwisha kujiandaa kwa huduma zote za uokoaji,” alisema Afisa Habari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Paschal Shelutete.
Shelutete amesema hii ni mara ya kwanza kabisa tukio hili la kuruka kutoka kilele cha Kilimanjaro kwa kutumia miamvuli kufanyika nchini na kwamba likifanikiwa litajumuishwa kuwa miongoni mwa vivutio vipya vya utalii.
Marubani hao walianza kupanda mlima tarehe 27 Januari na ilitarajiwa kuwa wangeruka kutoka kilele cha Uhuru siku ya tarehe 5, wakielea kutumia miamvuli hiyo maalum, ikiwa ni tukio la kwanza kabisa kufanyika nchini.
Mratibu wa taasisi ya ‘Wings of Kilimanjaro,’ ya Australia, inayoratibu zoezi hilo, Bi Paula McRae amesema zoezi hilo pia litasaidia kuchangia fedha kiasi cha dola millioni moja za kimarekani kwa ajili ya kusaidia jamii zinazounguka mlima huo mrefu zaidi barani Afrika.
DSCF7475
Picha ikionysha mwanamama aliyekuwa katika hali mbaya na kuamua kulala chini huku akimhofia mumewe alipanda mlima mara baada ya kupata taarika kuwa hali ya mlima huo bado ni tete
DSCF7473
Hapa ni baada ya heliKopta kurudi chini ambapo kamera ilifungwa na baadae kuleta hali halisi ya mlima huo …..hapa ndugu jamaa na marafiki wa marubani wakiwa wanaangalia video ya tukio hilo
DSCF7476
DSCF7470
Kikosi kazi cha waandishi wa habari walioweka kambi maalum kuwasubiri watalii kushuka kutoka mlima Kilimanjaro kwa kutimia miamvuli,zoezi ambalo halikuzaa matunda(picha zote na jamiiblog.co.tz)


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU