Facebook Comments Box

Thursday, February 7, 2013

SUNZU HATOKUWEPO MECHI YA SIMBA NA JKT OLJORO

UONGOZI wa Klabu ya Simba umethibitisha  kuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Felix Sunzu hatokuwamo kwenye msafara wa timu hiyo utakaoelekea Arusha kesho kwa ajili mechi ya ligi dhidi ya JKT Oljoro.
Akizungumza jijini Dar es Salaam msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga alimesema kuwa Sunzu ameondolewa katika kikosi  kitakachoivaa JKT Oljoro kutokana na kuwa majeruhi.
"Kama tulivyopanga awali kikosi chetu  kitaondoka kesho kuelekea Arusha kikiwa na wachezaji 20.
"Mpaka wakati huu mchezaji ambaye ninaweza kukuthibitishia kwamba hatokuwa miongoni mwa wale watakaosafiri ni Felix Sunzu ambaye bado anasumbuliwa na majeraha,".alisema Kamwaga.
Kamwaga alisema kuwa, orodha kamili ya wachezaji 20 watakaosafiri kuelekea Arusha ilitarajiwa kutangazwa mapema baada ya kumalizika kwa pambano kati ya Timu ya Taifa(Taifa Stars) na Cameroon leo jioni.
"Nani na nani watakuwamo katika kikosi kitakachosafiri itajulikana leo jionibaada ya mechi kati ya Taifa Stars na Cameroon kama unavyojua tuna wachezaji kwenye timu ya Taifa. Hatuwezi kujua kuna nini kitatokea baada ya mchezo,".alisema Kamwaga.
Pambano baina ya Simba na JKT  litapigwa Jumamosi hii kwenye Dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Katika pambano la mzunguko wa kwanza  lililopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Wekundu wa Msimbazi, Simba ilichomoza na ushindi wa mabao 4-1


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU