Facebook Comments Box

Sunday, January 27, 2013

UJUMBE WA SEKRETARIETI YA CCM WAWASILI SALAMA MKOANI KIGOMA LEO


 Wananchi wa Mkoa wa Kigoma leo wameupokea kwa shangwe Ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) uliowasili mkoani Kigoma ukitokea jijini Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa Treni Reli ya Kati.
Wajumbe hao ambao wanaoongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana ni pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM,Martin Shigela.
Akizungumza baada ya kuwasili Mkoani Kigoma leo, Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana alisema kuwa lengo la wao kutumia usafari huo wa Treni ni kuwadhihirishia wananchi wa Tanzania kuwa Usafiri wa Treni ni Usafiri wa uhakika na Serikali ya Chama cha Mapinduzi kupitia Wizara ya Uchukuzi, itasimamia kikamilifu usafiri huo na kuendelea kuuboresha zaidi ya ilivyo sasa na kuhakikisha safari zinaongezeka na kuwa za kila siku na si kuwa kwa wiki mara mili kama ilivyo sasa.Nao baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma wameipongeza sana Sekretarieti hiyo kwa uamuzi wao wa kusafiri kwa kutumia Treni kutoka jijini Dar es Salaam hadi Mkoani Kigoma na kujionea hali halisi ya usafiri huo.
Ujumbe huo upo Mkoani Kigoma kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanachama pamoja na wananchi wa mji wa Itigi mkoani Singida wakati Treni iliposimama kwa muda mfupi katika mji huo.


Wananchi wa Mkoa wa. kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi.


Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wakiwa wamekusanyika kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati akizungumza nao.

Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wakielekea kuupokea Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM wakati ukiwasili Mjini Kigoma leo.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Mji wa Kigoma waliofika kuupokea Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM uliowasili mjini Kigoma leo kutokea jijini Dar es Salaam kwa usafiri wa Treni ya Reli ya kati.



Katibu wa NEC, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa (CCM),Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na wananchi wa Mji wa Kigoma waliofika kuupokea Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM uliowasili mjini Kigoma leo kutokea jijini Dar es Salaam kwa usafiri wa Treni ya Reli ya kati.


Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akifurahia ngoma ya utamaduni ya mkoa wa Kigoma iliyokuwa ikipigwa Stesheni leo,huku Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akipiga moja ya ngoma hizo.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia) akipena mkono na Dereva wa Treni ya TRL,Bw. Kambi Ali (wa pili kulia) aliyewasafirisha kutoka Jijini Dar es Salaam mpaka Mjini Kigoma salama. Wengine pichani ni Katibu wa NEC, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa (CCM),Dkt. Asha-Rose Migiro pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM), Nape Nnauye.




Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU