Facebook Comments Box

Sunday, January 27, 2013

TAARIFA MPYA KUTOKA KUSINI: WALIOFARIKI WAFIKA 9, VIONGOZI WAWASILI

IDADI ya watu waliouawa katika vurugu za wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara imeongezeka na kufikia Tisa kutoka saba walioripotiwa awali. Mmoja aliyekuwa majeruhi na kulazwa hospitali ya misheni ya Ndanda ameripotiwa kupoteza maisha yake. Ndugu wa karibu wa marehemu amemthibitishia mwandishi wa kuwa ndugu yao amefariki leo saa 9 usiku akiwa anapatiwa matibabu hospitalini.
 Mchana wa leo, mwendesha bodaboda mmoja ameuawa kwa kupigwa na vitu vinavyosadikika kuwa ni risasi za moto na kupoteza maisha papo hapo. Wananchi wamedai polisi wakiwa katika gari walimminia risasi kijana huyo aliyekuwa anaendesha pikipiki yake. Haya ni mauaji ya kwanza kutokea kwa polisi kuua watu wengi kwa risasi za moto, hali inayoitia doa Serikali. Tayari Waziri wa Mambo ya Ndani, Emanuel Nchimbi amewasili mkoani Mtwara akiambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Saidi Mwema, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (JWTZ) Davis Mwamunyange. Habari zinasema kuwa viongozi hao watafaya kikao na viongozi wa Mtwara na badaye kwenda Masasi kushuhudia hali ilivyo. Hata hivyo kuna habari kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda atawasili kesho mjini Mtwara, kufuatia vurugu zinazoendelea ambazo zinachagizwa na kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam. 

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU