Baada ya kipigo cha mara mbili mfululizo kutoka kwa timu 
ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, timu ya Black Leopards ya nchini 
Afrika ya Kusini, leo imepunguza machungu yake kwa kuichapa Simba ya 
jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0, katika mchezo wao wa kirafiki wa 
kimataifa uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
Hata
 hivyo imeelezwa kuwa kutokana na hofu Klabu ya Simba iliwachezesha 
wachezaji wa timu B, jambo ambalo limewakera hadi mashabiki wa Simba 
waliokuwapo uwanjani hapo leo, ambapo baadhi ya mashabiki waliohudhuria 
mtanange huo uwanjani hapo walisikika wakilalama kwa kitendo hicho, 
ambacho kimeelezwa kuwa ni sehemu ya hofu na dharau.
Katika
 Kikosi cha simba wameonekana wachezaji wanne tu walio katika kikosi cha
 kwanza cha ligi kuu. huku wachezaji wote waliobaki wakiwa ni wa kikosi 
cha pili, ambao wengi wao wakiwa ni wchezaji wa kikosi cha timu B ya klabu hiyo.
Simba kupitia makamu mwenyekiti wake Godfrey
 Nyange Kaburu jana ilithibitisha kwamba watachezesha kikosi cha kwanza 
baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba walikuwa na mpango wa kutaka 
kuchezesha kikosi cha pili cha timu hiyo, lakini Kaburu alizungumza 
kwenye Sports Xtra ya Clouds FM na kuthibitisha kwamba kikosi 
kilichotoka Oman ndio kitakachoshuka dimbani kupambana na Black 
Leopards.
Kitendo ilichokifanya Simba sio cha kiungwana kwa sababu imehairibia jina kampuni iliyoratibu mchezo huo ya Prime time promotions, ambao
 walitimiza kila kitu katika makubaliana yao na Simba ili wailete timu 
ya kwanza kucheza na Black Leopards lakini matokeo yake wakafanya 
kinyume na makubaliano.  
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
