Facebook Comments Box

Thursday, January 24, 2013

LULU KUACHIWA KWA DHAMANA KESHO IJUMAA 25/01/2013

. 
 Taarifa za uhakika zilizopo kwa sasa ni kwamba kuna uwezekano mkubwa mwigizaji Elizabeth Michael maarufu kwa jina la uigizaji 'Lulu' akatoka kwa dhamana kesho January 25, 2013. Kutokana na dhamana ambayo inatarajia kusikilizwa kesho Ijumaa.

Uhakika wa Lulu kupata dhamana ulikua jana jumatano january 23 lakini ikashindikana kutokana na kuahirishwa kwa sababu Jaji alipata dharura na pia kiwango cha pesa za dhamana kilikua hakijatimia.
Chanzo cha kuaminika kilichoongea kimesema dhamana ya kumtoa Lulu ambae amekua chini ya ulinzi kuanzia April 2012 ni milioni 20 za kitanzania.

Lulu amekua akishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwigizaji Steven Kanumba, na baadae mashitaka yake yalibadilishwa na kuwa Ameua bila kukusudia, kitu ambacho kinampa nafasi ya kuweza kupata dhamana.




Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU