Facebook Comments Box

Saturday, January 26, 2013

KITABU KIPYA CHA ADAM SHAFI (MWANDISHI WA KULI) KIMETOKA


 
Juma hili habari kwamba kitabu kipya cha mwandishi nguli, Adam Shafi (mwandishi wa vitabu vya Kasr ya Mwinyi Fuad, Kuli, Vuta Nkuvute na Haini) kimetoka ni za kushangilia sana.

“Mbali na Nyumbani” inaangalia maisha yake msanii huyu Ughaibuni takribani miaka 50 iliyopita.

Mara ya mwisho nilipomhoji Mzee Shafi, Desemba 2007 alikuwa bado anakiandika kitabu hicho ambacho alisema kitaelezea maisha yake ya ujanani.

Katika uchambuzi wa kitabu hicho, mwandishi hodari wa Kenya, Profesa Ken Walibora, anasema mtindo wake wa kuangalia tawasifu- ambapo mwandishi au mhusika anaelezea maisha yake haujaenea sana katika maandishi ya Kiswahili seuze ya Kiafrika. Hivyo anasema Walibora, ni jambo zuri la sisi wengine pia kulifanya.

Mbali na kutukuza kitabu hiki, Profesa Walibora anachangamkia namna maandishi na lugha ya Kiswahili inavyoendelea kukua duniani. Hivyo, kututaka Waswahili kuendelea kuandika na kujenga na kuimarisha KISWAHILI.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU