Yanga
 na Tanzania Prisons zimeingiza mapato ya jumla ya sh. 101,016,000 
katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara
 iliyofanyika jana (Januari 28 mwaka huu).
Mechi
 hiyo namba 94 ilichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Yanga kuibuka
 na ushindi wa mabao 3-1. Watazamaji 17,946 walikata tiketi kushuhudia 
pambano hilo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 
20,000.
Watazamaji
 16,158 kati ya hao walikata tiketi za sh. 5,000 wakati idadi ndogo ya 
washabiki ilikuwa ni 98 waliokata tiketi za sh. 20,000.
Kila
 klabu imepata mgawo wa sh. 24,314,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la 
Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 15,409,220.34. Asilimia 15 iliyokwenda 
kwenye uwanja baada ya kuondoa VAT na gharama za tiketi ni sh. 
12,363,433.45.
Mgawo
 mwingine wa mapato hayo ni tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 
7,413,060.07, Kamati ya Ligi sh. 7,418,060.07, Mfuko wa Maendeleo ya 
Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,709,030.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa 
wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,884,801.14.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
