Mvua 
kubwa iliyonyesha morogoro jioni ya leo imesababisha mafuriko katika 
mtaa wa morogoro.Mvua hiyo iliyoanza kunyesha kuanzia saa tisa alasiri 
imenyesha takribani kwa masaaa mawili imesababisha mafuriko katika 
barabara ya msamvu kuingia katikati ya mji hali iliyosababisha msongamano
 mkubwa wa magari.
 Maji yakiwa yamejaa eneo la mtawala baada ya mvua kubwa kunyesha jioni hii mkoani morogoro
 Mafuriko
 hayo yaliingia katika makazi ya watu na hapa ni mashine za kukoboa 
mpunga wakiwa wamesimamisha kazi zao baada ya maji kuingia ndani.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog