Basi la Yanga |
BASI la Yanga limefanyiwa fujo na watu wasiojulikana, wanaosadikiwa
kuwa ni mashabiki wa Simba, eneo la Kabuku, wakiwa njiani kuelekea Tanga.
Baraka Kizuguto, Ofisa tovuti wa Yanga aliye katika msafara
wa timu ameiambia kitongoni mida hii kwamba, jamaa aliyerushwa jiwe alikuwa juu
ya mti na limepasua kioo, ila halijajeruhi mtu.
Amesema wametoa ripoti Polisi, ingawa hawakufanikiwa kumkamata
mtu kwa sababu wahusika walikuwa wamekwishakimbia baada ya tukio.
Yanga iliyoondoka leo alfajiri Dar es Salaam tayari ipo Tanga
, imefikia katika hoteli ya Central City, barabara ya Nane na jioni itafanya
mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana.
Yanga iko Tanga kwa ajili mchezo wao wa mwisho wa mzunguko wa
mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji
Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumapili.
Yanga imepania kushinda mechi hiyo ili kujiweka katika
mazingira mazuri katika msimamo wa Ligi Kuu, ambayo mzunguko wake wa pili
utarejea Januari mwakani.
Yanga ilifanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa
sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam jana na wachezaji wake wote wapo
vizuri, chini ya kocha wake Mholanzi, Ernie Brandts.
Wchezaji wa
Yanga wamepania kuvunja rekodi ya Coastal Union kutofungwa kwenye Uwanja wao wa
nyumbani, Mkwakwani, Tanga katika mechi hiyo.
Akizungumza
na kitongoni kwa niaba ya wenzake mapema wiki hii, Nahodha Msaidizi wa
Yanga, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ alisema kwamba wanataka kustawisha uongozi
wao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kuwafunga Coastal Jumamosi.
Alisema
wanajua Coastal ni timu nzuri na wanatarajiwa upinzani katika mechi hiyo, ila
ameonya Yanga ya sasa ni tishio na wachezaji wako vizuri ‘ile mbaya’.
“Kwa kweli
mimi na wachezaji wenzangu tunamshukuru mwalimu mpya (Ernie Brandts) kwa kutupa
vitu vipya na muhimu. Timu yetu imebadilika na kila mtu anaona sasa. Wale
Coastal si hawafungwi kwao wale, sasa sisi tutaenda kuwafunga pale pale, tena
kipigo kikali,”alisema.
Lakini pia
habari za ndani kutoka Yanga zinasema kwamba tayari wachezaji wameahidiwa donge
nono iwapo watashinda mechi hiyo.
Wachezaji
hao, walizawadiwa Sh. Milioni 15 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC mwishoni
mwa wiki katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Ushindi huo,
uliifanya Yanga iongoze Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 26, ikiwa imebakiza mechi
moja ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Caostal Union mjini Tanga, ikifuatiwa na
Simba SC yenye pointi 23, ambayo juzi imefungwa 2-0 na Mtibwa Sugar mjini
Morogoro.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog