Facebook Comments Box

Wednesday, September 26, 2012

TOVUTI ZA SIMBA NA YANGA ZAFUNGWA
















Katika hali ya kusikitisha na kushangaza zile tovuti za klabu kubwa za mpira hapa Tanzania za Yanga na Simba leo zimekuwa hazipo hewani. Watu mbalimbali ambao wamekuwa wakizitafuta kupata habari za klabu zao hizo kongwe. Wamekuwa wakikuta ujumbe unosema "This account has been suspended"
Baadhi ya wataalamu wa mambo ya mawasiliano wanasema hali hiyo itakuwa inatokana na kushindwa kulipia gharama za tovuti hizo kuwepo hewani. Tovuti ya yanga ni www.youngafricans.co.tz na ile ya watani wao wa jadi ni www.simba.co.tz
Juhudi bado zinafanyika kujua nini sababu ya tovuti hizo kutokuwepo hewani zote kwa pamoja kwa wakati mmoja. Ikumbukwe klabu hizi mbili ndio zinaongoza kwa kuingiza mapato na pia zina udhamini mnono.

OKWI KUIKOSA MECHI YA YANGA

Taarifa nilizozipata usiku huu kamati ya ligi iliyokutana leo imemfungia mshambuliaji wa Simba,Emmanuel Okwi michezo mitatu pamoja faini ya tsh 500,000 kutokana na kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo dhidi ya JKT RUVU kwa kosa la kumpiga kiwiko Kessy Mapande.
Kutokana na adhabu hiyo Emmanuel Okwi ataukosa mchezo dhidi ya Yanga. 

 HIVI NDIVYO ALIVYOPATA KADI NYEKUNDU






Tuesday, September 25, 2012

ZIMWI LA YANGA LAIKUTA COAST UNION. KOCHA WAO KIBARUA CHAOTA NYASI

Juma Mgunda akiokolewa na polisi kuondoka uwanjani kwa amani baada ya mechi ya Bandari
Baada ya kunusurika kupigwa na mashabiki katika mechi ya kirafiki dhidi Bandari ya Mombasa, na kuendelea kupewa presha kubwa na mashabiki wa timu yake ya Coastal Union hatimaye kocha wa klabu hiyo yenye maskani yake jijini Tanga Juma Mgunda ametangaza kujiuzulu kuifundisha timu hiyo baada kuiongoza timu kwenye mechi zisizozidi nne kwenye ligi kuu ya Tanzania bara.

Mgunda ambaye alipewa kibarua cha kuifundisha Coastal Union kipindic ha kiangazi kilichopita amesema ameamua kujiuzulu kutokana na presha kubwa anayopewa mashabiki kiasi cha wengine kutishia usalama wake.

Mgunda ameiongoza Coastal katika mechi 3 za ligi, akishinda moja na wakitoa suluhu mechi mbili.



MCHUNGAJI MTIKILA ASHINDA KESI

Picture
Mchungaji Christopher Mtikila akifurahia ushindi baada ya kushinda kesi dhidi yake.
MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameshinda kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili.

Akizungumza baada ya kushinda kesi hiyo, Mtikila amesema, "Ushindi huu niliutarajia maana hata asubuhi kabla ya kuja mahakamani niliongea na Yesu na sasa amenijibu".

Mara baada ya kushinda kesi hiyo lilizuka timbwili lingine baada ya mtu mmoja kujitokeza akiwa na RB (Report Book) akimtuhumu Mchungaji Mtikila kuwa alimtishia kumuua na ni mwizi wa viwanja. Baada ya kutaka kukamatwa na polisi mmoja aliyekuwa na cheo cha Koplo, Mchungaji alikataa kwa madai kuwa yeye ni kiongozi wa kitaifa hivyo hawezi kukamatwa na polisi mwenye cheo cha Koplo, labda polisi mwenye cheo cha SSP (Senior Superintendent of Police). Kwa kauli hiyo polisi alishindwa kumtia nguvuni.

Picture
Mtikila amkimsikiliza Koplo wa Polisi mwenye RB Namba : KMR/RB/10482 yenye maelezo ya kutishia kuuwa kwa maneno na wizi wa viwanja iliyofunguliwa na bwana Gotta Ndungulu.
* "Hukumu dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, iliyoahirishwa mara mbili kwa sababu ya hakimu kuwa na dharura, ilisomwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu a Hakimu Mkazi Mfawidhi, Illivin Mugeta aliyeisikiliza kesi hiyo ya kutoa maneno ya uchochezi.

Mtikila alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya kusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete, kwamba anataka kuuangamiza Ukristo.

Mshitakiwa Mtikila alifunga ushahidi kwa kuwa na mashahidi wawili wa utetezi, akihofia kupoteza fedha za Serikali kwa kuwaleta mashahidi wengi ambao hawana kitu tofauti na mashahidi wengine waliokuwa wamewasilisha ushahidi wao mahakamani hapo.

Mtikila, anadaiwa kwamba, Aprili, 2010 Dar es Salaam, alisambaza waraka aliokuwa akidai ni wa kuunusuru Ukristo wenye lengo la kuangamizwa na Jihad ya Rais Jakaya Kikwete na kwamba Wakristo wajitoe mhanga kukomesha ugaidi, “Kikwete anaangamiza Ukristo, amekuwa jasiri wa kuingiza Uislamu katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alidai Mtikila katika waraka wake huo.

Alidai waraka uliosambazwa alisaini akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kuunusuru Ukristo na walichapisha nakala 100,000, lakini aligoma kutaja mahali walipochapishia nakala hizo. Maelezo yote hayo yalitolewa mahakamani kama kielelezo na ofisa wa polisi, SSP, Ibeleze Mrema aliyemuhoji Mtikila Aprili 14, 2010."



HAKIMU KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

 

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala Pamela Kalala (kushoto),akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana,baada ya kusomewa shitaka la kuomba rushwa ya Shilingi milioni tatu. 
HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Pamela Kalala amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, kujibu mashitaka ya kuomba rushwa Sh milioni 3 na kupokea Sh 900,000.

Kalala alipandishwa kizimbani jana mbele ya Hakimu Aloyce Katemana na kusomewa mashitaka yanayomkabili. Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Allen Kasamala alidai kuwa mshitakiwa anakabiliwa na mashitaka matatu.

Kwa mujibu wa Kasamala katika tarehe tofauti Februari mwaka huu mshitakiwa akiwa katika Manispaa ya Ilala aliomba rushwa ya Sh milioni 3 kutoka kwa Josephine Wage. Wage ni mke wa mshitakiwa katika kesi namba 703 ya mwaka 2008, dhidi ya Aboubakar Hamis na wenzake, na alitaka kumshawishi ili atoe uamuzi wa kumpendelea mumewe katika kesi inayomkabili.

Katika mashitaka la pili, Kalala anatuhumiwa kupokea rushwa ya Sh 800,000 kutoka kwa Wage, ikiwa ni ushawishi wa kutoa uamuzi wa kumpendelea mume wake huyo.

Hata hivyo, Kasamala alidai kuwa katika mashitaka ya tatu, hakimu huyo anatuhumiwa kupokea rushwa ya Sh 100,000 kutoka kwa Wage Februari 6, ukiwa ni ushawishi wa kutoa uamuzi wa upendeleo.

Mshitakiwa alikana mashitaka yote na Kasamala kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na upande wa Jamhuri hauna pingamizi juu ya dhamana.

Katemana alisema ili mshitakiwa aweze kuwa nje kwa dhamana, anatakiwa asaini hati ya dhamana ya Sh milioni moja na mdhamini mmoja wa kuaminika atakayesaini hati ya dhamana ya kiasi hicho cha fedha.

Mshitakiwa alikidhi masharti ya dhamana na kuwa nje hadi Oktoba 23 kesi hiyo itakapotajwa.

Baada ya kutimiza mashati hayo, Kalala akifuatana na mtu anayedaiwa kuwa mumewe, walitoka mahakamani hapo kwa kupitia mlango wa nyuma kwa lengo la kukwepa wapigapicha waliokuwa wakisubiri picha yake. Hata hivyo, wapigapicha hao walimwona na kumkimbilia ili kumpiga picha, hata hivyo waliendelea kupata ugumu baada ya mumewe kumkumbatia huku akicheka kwa dharau na kuwataka wapige picha kadri wawezavyo.


WIZI WA VIFURUSHI VYA ABIRIA NA WATEJA JK NYERERE AIR PORT




Monday, September 24, 2012

Thursday, September 20, 2012

MADEREVA WA BODABODA ARUSHA WAFANYA VURUGU

Picture
Dereva pikipiki ambaye hakujulikana mara moja jina lake akitaka kupasua kioo cha gari dogo baada ya dereva wa gari hilo kutaka kupita eneo walilozuia.
MADEREVA pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zaidi ya 300, jijini Arusha wameandamana na kufunga barabara kuu ya Moshi-Arusha kwa zaidi ya saa 3, katika eneo Ngulelo, wakilituhumu jeshi la polisi kumwachia mtuhumiwa wa mauaji anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi mwenzao bila hatia.

Madereva hao wakiwa na pikipiki zao, walifunga barabara hiyo kuanzia majira ya  saa 4  asubuhi hadi saa 6 mchana kwa mawe na magogo hali iliyolazimu jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia kuingilia kati na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na risasi za moto .

Kwa mujibu wa mmoja wa waendesha pikipiki, Jonathan Emanuel, Mkazi wa Ngulelo wilaya ya Arumeru, maandamano hayo yalilenga kulaani mauaji ya mwenzao aliyemtaja kwa jina la Hilari Elias (36) mkazi wa Oldadai, aliyeuawa kwa kupigwa risasi  Septemba 15 mwaka huu akiwa barabarani  eneo la Baraa akimsafirisha abiria aliyekuwa amemkodi.


Madereva hao wakiwa na mabango  yenye ujumbe mbalimbali  wa kulaani jeshi la polisi kumwachilia mtuhumiwa wa mauaji (jina linahifadhiwa) anayedaiwa kuwa na uwezo wa kifedha na mmiliki wa garage ya kutengeneza magari  na mkazi wa Baraa, walilituhumu jeshi la polisi mkaoni hapa kwa kucheza mchezo mchafu wa kumwachulia mtuhumiwa aliyempiga risasi dereva mwenzao na kumsababishia kifo chake.

Maandamano hayo yalianzia katika kituo cha basi eneo la Ngulelo majira ya saa 2 asubuhi kuelekea mjini katika chumba cha maiti katika hospitali ya mkoa Mount Meru kuuchukua mwili wa merehemu na baadaye yalielekea nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo madereva hao kwa pamoja  walivunja lango la kuingilia na kuharibu mali za mtuhumiwa ikiwemo gari lake  lililovunjwa vioo vyote pamoja na vyoo vya nyumba hiyo.

Aidha baada ya tukio hilo madereva hao walifunga barabara katika eneo la Ngulelo kwa mawe na magogo wakishinikiza  mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo kufika eneo hilo na kuwasikiliza kwani walikuwa hawana imani na jeshi la polisi huku wakidai ya kuwa mtuhumkiwa wao naonekana akirandaranda mitaani.

Katika eneo hilo pamoja na kufunga barabara hiyo,madereva hao  walivunja vioo vya magari kwa kupiga  mawe vioo vya magari na kuharibu baadhi ya magari yaliyokuwa yakijaribu kupita kwa nguvu wakati wamefunga barabara hiyo,huku wakipaza sauti kwa kupiga yowe wakiwa wamelala barabarani huku wakitaka mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo afike kuwasikiliza kilio chao kwani hawana imani na jeshi la polisi.

Tukio hilo limethibitishwa na kamanda wa polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabasi na kueleza kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi hapo baadae,na mwili wa merehumu huyo umezikwa na umati mkubwa wa watu nyumbani kwap eneo la Oldadae.



Jaji Mkuu, Othman Chande aahirisha kesi ya rufaa ya Godbless Lema



 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande ameahirisha kesi ya rufaa ya aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, hadi Oktoba 2, 2012 kwa mujibu wa maombi ya mawakili wa pande zote mbili, CCM na CHADEMA walioandika barua ya kuomba kuahirishwa kwa kesi hiyo baada ya kifo cha mzazi  wao ambaye maziko yake yanatarajiwa kufanyika Septemba 22, 2012.

Jaji Mkuu ametoa amri fupi ya Mahakama kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alikuwa anajibu maombi wa pili aunganishwe kama mtu muhimu katika kesi hiyo.

Kesi hiyo ambayo imesikilizwa kwa takribani saa mbili chini ya Jaji Mkuu na Majaji wengine wawili wa Rufani, ni ya kukata rufaa kupinga kuvuliwa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).

Mara baada ya kesi hiyo kuhairishwa, umati mkubwa uliokuwepo mahakamani hapo uliondoka hadi katika ofisi za CHADEMA ambapo Lema aliongea na wananchi waliokuwa wakimsindikiza na kuwasihi kuwaombea Majaji wa kesi hiyo ili waweze kutoa hukumu ya haki, “mimi sio kwamba nataka nishinde na wala siogopi kushidwa ila naomba tuwaombe hawa majaji wa kesi hii ili waweze kutoa maamuzi ya haki yasiyomgandamiza mtu yeyote,na napenda pia kuchukuwa nafasi hi kuwaeleza kuwa jumanne tunatarajia kufanya mkutano katika kiwanja cha ngarenaro ambapo hapo ndipo tutakapo fungua kampeni zetu za udiwani rasmi,” alisema Lema.

Katika kesi hiyo, Lema anatetewa na Tundu Lissu, wakati kaka yake, Alute Mughwai, anawatetea walalamikaji.

Wakili Mughwai anashirikiana na wakili Modest Akida kuwawakilisha wadaiwa kwenye shauri hilo ambao ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dkt. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi.

Awali, Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu, aliwasilisha kwenye mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.

Kwenye baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.

Aidha, aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Katika madai mengine, Lema anamlalamikia Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo kuwa alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Lema anadai kuwa jaji alikosea wakati alipoamua kuwa mpiga kura yeyote anaruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.

*picha zimepatikana kwenye blogu ya "Libeneke la Kaskazini"

Picture
Umati wa wakazi wa Arusha waliofika eneo la Mahakama Kuu kusikiliza rufaa hiyo.
Picture
Wananchi wakiwa nje ya ofisi ya chama wanamsikiliza Lem


Tuesday, September 18, 2012

RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA BARABARA YA MSATA-BAGAMOYO

Picture
Rais Dk Jakaya Kikwete (katikati) akiweka jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo - Msata uliofanyika katika kijiji cha Kiwangwa wilayani Bagamoyo leo mchana. Wengine katika picha kutoka (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi, Kaimu Mkuu wa mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik (wa pili kushoto), Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (wanne kushoto) na kulia ni Waziri wa Mazingira Mh Terezya Huviza. (Picha: Freddy Maro/IKULU)


                                TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ndoto ya miaka mingi ya kujengwa kwa barabara ya Msata-Bagamoyo kwa kiwango cha lami imetimia leo, Jumanne, Septemba 18, 2012, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipoweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara hiyo katika sherehe kubwa iliyofanyika eneo la Kiwangwa.

Barabara hiyo ya kilomita 64 inajengwa na mkandarasi wa ndani ya nchi, Estim Construction, na inagharimiwa asilimia mia na Serikali ya Tanzania bila msaada kutoka kwa mfadhili yoyote.

Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania, Injinia Patrick L. Mfugale amesema kuwa barabara hiyo inayogharimu kiasi cha Sh. bilioni 94, ikiwa ni pamoja na fedha za fidia na kumlipa mkandarasi mshauri, itakamilika Juni mwakani.

Pamoja na kwamba Mheshimiwa Rais ameweka jiwe la msingi kwenye barabara hiyo, Injinia Mfugale amesema kuwa mkandarasi wa sasa alianza ujenzi tokea 2010 baada ya usanifu wa barabara hiyo kukamilika na baada ya Serikali kumtimua mkandarasi wa mwanzo wa barabara hiyo, TACOPA, Novemba 13, mwaka 2009.

Amesema kuwa mpaka sasa barabara hiyo imekamilika kwa asilimia 65, yaani kwamba kiasi cha kilomita 36.7 tayari zimewekwa lami na kuwa ni kilomita 23 zilizosalia na ambazo zitamalizika katika miezi tisa ijayo.

Injinia Mfugale amesema kuwa mpaka sasa Serikali imekwishakulipa kiasi cha Sh. bilioni 56.8 ikiwa ni pamoja na fedha iliyolipwa kama fidia kwa wananchi ili kupisha ujenzi wa barabara hiyo.

Amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo hautahusisha ujenzi wa daraja kwenye Mto Ruvu kwa sababu usanifu wa daraja hilo ulichelewa kidogo kukamilika hata kama tayari sasa umekamilishwa.

Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa John P. Magufuli amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo ni sehemu ya ujenzi wa kilomita 11,154 za barabara za lami zinazojengwa na Serikali ya Mheshimiwa Kikwete.

“Nataka muelewe vizuri maana ya kilomita hizi. Wakati wa Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, tulikuwa na barabara za lami zenye urefu wa kilomita 1,330. Kati ya Uhuru na mwaka 2005, tulijenga barabara zenye urefu wa kilomita 6,500 na kati ya 2005 na sasa tunajenga barabara zenye urefu wa kilomita 11,154,” amesema Waziri Magufuli.

Waziri huyo amerudia msimamo wake kuwa kamwe Serikali haitawaachia watu wanaojenga ama kufanya shughuli katika eneo la hifadhi ya barabara bila kuwachukulia hatua.

Naye Rais Kikwete amewaambia mamia kwa mamia ya wananchi walioshiriki katika sherehe hizo kuwa barabara ndiyo mishipa ya damu ya uchumi wa nchi yoyote na ndiyo maana Serikali inatenga kiasi kikubwa katika Bajeti yake kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Amesema kuwa katika Bajeti ya sasa, barabara zimetengewa kiasi cha Sh. trilioni 2.2 ambacho ni kiasi kikubwa cha pili baada ya Bajeti ya elimu.

Rais Kikwete amesema kuwa pamoja na faida zake kubwa na nyingi, barabara hiyo itakuwa na changamoto zake ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ajali za barabara, kuongeza urahisi wa kusambaa kwa ugonjwa wa ukimwi na hata kuvutia watu wenye lengo la kununua ardhi kubwa ya wanavijiji ambako inapita barabara hiyo.

Rais pia ameungana na Waziri Magufuli kwa kuonya: “Kama alivyosema Waziri, wanaoifuata barabara watavunjiwa nyumba zao na hawatalipwa, lakini wale ambao barabara inawafuata watalipwa hata wakivunjiwa.”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

18 Septemba, 2012
Picture
Sehemu ya Barabara ya Bagamoyo - Msata iliyojengwa kwa kiwango cha lami ambayo ujenzi wake ulizinduliwa rasmi leo na Rais Dk Jakaya Kikwete, huko Kiwangwa, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. (Picha: Freddy Maro/IKULU)


RAIS OBAMA AJIBU BARUA YA MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI YA UGANDA


Kijana Christopher Kule na babake Dasiel Raul
Kama kuna rais ambaye watu wengi Uganda wangetaka kukutana naye ni rais wa Marekani Barack Obama.
Kijana Christopher Kule, mwenye umri wa miaka kumi na ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi wilayani Kasese, nchini Uganda, hajaachwa nyuma katika ndoto hiyo.
Bila shaka wengi watasema yuko hatua nyingi mbele ya wale walio na ndoto ya kumuona Obama. Hii ni baada ya Kule kupokea majibu ya barua aliyomwandikia Rais Barack Obama kutoka kwa Obama mwenyewe.
Kijana huyo anaamini kuwa baada ya kuandikiana barua na Rais Obama, kuna matumaini kwamba siku moja atakutana naye.
Yote haya yanatokana na zoezi la kuandika barua ambalo Kule na wanafunzi wenzake walikuwa wanafanya darasani, baada ya kuagizwa na mwalimu wamwandikie barua mtu yeyote wakiomba msaada kwa jamii yao.
Barua ya Kule bila shaka ilimtia hamasa mwalimu wake wa kigeni kutoka Marekani ambaye alikuwa anafunza shuleni humo kwa muda.
Mwalimu huyo alisema kuwa nyanyake ni rafiki wa mmoja wa wasaidizi katika ikulu ya rais na kuahidi kuhakikisha kuwa ujumbe huo utamfikia rais Obama na bila shaka ahadi ikatimizwa , kwani barua ilimfikia rais Obama.
Kule alisema kuwa katika barua yake, alimwomba Obama kusaidia Uganda kuangamiza uasi na kuhamasisha amani.
Katika majibu yake kwa Kule, rais Obama alisema kuwa Marekani imejitolea kuangazia maswala kadhaa muhimu kote duniani kama haki za binadamu kwa sababu Marekani inapinga vikali ghasia na ukandamizaji dhidi ya watu wote. Pia alimtumia kijana huyo picha yake aliyokuwa ametia saini.

TAMKO LA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA

KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA JUU YA UTEKELEZAJI WA MADAI YA MADAKTARI NCHINI TAREHE 18.09.2012


Kamati ya Jumuiya ya Madaktari Nchini , kwanza inapenda kutoa pole kwa Wanahabari wote nchini kwa kitendo cha kinyama ambacho Mwanaharakati na Mwandishi wa habari, Marehemu David Mwangosi alifanyiwa, hii ni ishara kuwa Jeshi la Polisi wameamua kutumia njia ya kuua raia ili kujenga hofu na woga miongoni mwa wapenda demokrasia na maendeleo nchini.

Pia tunapenda kulaani kitendo cha Serikali kupitia Wizara ya Michezo, Habari na Utamaduni kulifungia gezeti makini la Mwanahalisi kwa sababu ya kutoa taarifa za ukweli juu ya waliotaka kukatiza uhai wa Dr.Ulimboka Stephen, Jamii ya Madaktari na watanzania wengi bado wanaamini kuwa waliotajwa na gazeti la Mwanahalisi ni miongoni mwa waliohusika na kutekwa, kuteswa na kutelekezwa kwake na si yule anayesemekana kuwa na matatizo ya akili aliyedaiwa kukamatwa na Suleimani Kova. Hivyo tunalitaka Jeshi la Polisi litoe ripoti yake ya Uchunguzi ili kubaini ukweli wa taarifa hii.

Pia, tunachukua nafasi hii kupongeza mshikamano ambao Madaktari wameendelea kuuonyesha licha ya changamoto nyingi tunazopitia, ni vema ikafaamika kuwa ni katika kipindi hiki ambacho Mwenyekiti wa MAT na MAT imefunguliwa kesi 2 mahakamani, Ni katika kipindi hiki ambacho zaidi ya interns 300 wanasubiri kuitwa kuhojiwa na MCT bila kujua ni lini hilo litafanyika, Ni katika kipindi hiki ambacho Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari anapata mapumziko baada ya kutoka katika Matibabu nchini Afrika Kusini, lakini ni katika kipindi hiki ambacho mpaka sasa hakuna hata hoja moja ya Madaktari imefanyiwa kazi na Serikali.

Tunapenda ieleweke kuwa suala la madai ya Madaktari si tukio, ni mchakato ambao utaendelea kwa vizazi vya sasa na vijavyo, ndio maana tumeshuhudia migomo hii katika nyakati tofauti pamoja na kujitokeza kikundi au mtu kutumiwa kuomba msamaha kwa lengo la kudhalilisha taaluma na kurudisha nyuma jitihada za kuboresha hali ya afya nchini na maslai ya watumishi kwa ujumla.

Kuhusu suala la interns, Ikumbukwe kwamba mnamo tarehe 10, Julai 2012, Baraza la Madaktari Nchini lilitoa taarifa kwa umma kuwa imesitisha leseni za muda kwa Madaktari waliochini ya mafunzo kwa vitendo, pia waliahidi kuwaita kwa nia ya kuwahoji mmoja mmoja pindi wakatapokamilisha uchunguzi wao, cha kushangaza ni kwamba miezi 2 sasa imepita bila hilo kufanyika.

Katika vikao mbalimbali ambavyo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Naibu wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, na Kaimu Katibu Mkuu wameshiriki, wamekuwa wakisisitiza kuwa hili lipo kisheria na interns wasuburi kuitwa kwa ajili ya kuhojiwa. Hivyo tunapenda kutumia nafasi hii kuitaka MCT itekeleze kwa haraka majukumu yake kwa lengo la kuharakisha upatikanaji wa haki.

Hivyo basi Kamati ya Jumuiya ya Madaktari imejiandaa vya kutosha na taratibu za kisheria na itahakikisha inaweka wakili pale interns watakapoanza kuhojiwa kwa kuwa sheria inayounda MCT inatoa hiyo nafasi.

Mwisho kabisa tunapenda kutoa wito kwa interns kutumia hekima na busara katika kipindi hiki kigumu, waepuke kutumiwa na kikundi cha watu ambao wanatumika au wanajitumia kwa maslai ya kustarehesha watawala.

                           IMETOLEWA NA; KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA.



Monday, September 17, 2012

iPHONE 5 ZAUZWA MILIONI 2 NDANI YA MASAA 24

Kampuni ya Apple imesema imeuza simu yake mpya aina ya iPHONE 5 milioni 2 ndani ya masaa 24 baada ya kuizindua duniani kote. Mauzo hayo ni oda zilizotolewa kabla ya simu hiyo kuzinduliwa (pre oder). Vilevile kampuni hiyo imesema haitabadili siku ya kuitoa rasmi kwa wateja wake hao. Imebainisha kuwa itapeleka kwa wateja hao tarehe 21 septemba mwaka huu.




MWAKYEMBE AENDA KUINGIA MKATABA BERLIN

Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe na ujumbe wake wapo Berlin kuanzia tarehe 15 hadi 19 septemba kwa ziara ya kikazi. Moja ya tukio muhimu atakalo lifanya huko ni kusaini mkataba wa ushirikiano wa usafiri wa anga (Bilateral Air Service Agreement- BASA) baina ya nchi ya Tanzania na Berlin tarehe 17 septemba 2012. Tarehe 16 septemba Mheshimiwa alitembelea maonesho ya kimataifa ya sekta ya usafiri wa anga yaliyofanyika Berlin.
Mh Mwakyembe akiwa ndani ya moja ya ndege zilizokuwa kwenye maonesho hayo

Mh akipata maelezo kutoka kwa wataalam wa ndege za Airbus

Mh Mwakyembe akipiga picha na Balozi wa Tanzania Berlin Mh Ahmada (kushoto) na Afisa wa wizara ya uchuzi Ndg Ubwa (kulia)


Mh waziri akifanya mazungumzo na viongozi wa sekta ya anga wa Berlin



NYUMBU WARUDI SERENGETI KUTOKA MAPUMZIKONI






Msafara maarufu kwa jina la "Annual Animal Migration" unaohusisha wanyama aina ya Nyumbu wakiwa wanarudi katika mbuga ya Serengeti ya Tanzania wakiwa wanatoka katika mbuga ya Masai mara ya Kenya. Nyumbu hao walisafiri umbali wa zaidi ya kilometa 1000 katika mapumziko yao hayo. Msafara huo ambao ni maarufu zaidi duniani umevuta watalii wengi. Mwaka huu Nyumbu hao wamewahi kurudi kutokana na mvua zilizowahi kunyesha nchini Tanzania ambazo zimewawekea mazingira mazuri ya chakula. Nyumbu hao hukutana na mikasa na mazingira magumu wakati wa safari yao hiyo ambapo huwabidi kukatiza katika mto ambao una mamba na viboko ambao nao huwafanya msosi. Nyumbu hao waliorudi wanakaribia kuwa zaidi ya milioni moja na laki tano na huu ni msafara wa awali.

PICHA ZA UCHAGUZI MDOGO BUBUBU

Polisi wa kutuliza ghasia akimzuia mwananchi

Waangalizi wa usalama wakiwa kazini


Mawakala wa vyama wakifuatilia zoezi zima la upigaji kura

Mmoja ya wanasiasa akiongea na waandishi wa habari



Sunday, September 16, 2012

CHAMA CHA MAPINDUZI CHA SHINDA UBUNGE JIMBO LA BUBUBU

Matokeo ya kura za Ubunge jimbo la Bububu







Chama Mgombea Ubunge Kura %

1
CCMMasolwa Masolwa COSMAS 5,29656.3%
2
CUFSoud Khamis RASHID 3,80440.4%
3
JAHAZIIdrissa Mohammed ALI 550.58%
4
SAURashid Ali ALI 170.18%
5
TADEASalum Seif SEIF 160.17%
6
UPDPSaid Ahmad ASHA 120.12%
7
PPTOmar Said AYOUB 90.09%


ZILIZOHARIBIKA1952.07%


Jumla9,404








BREAKING NEWSS! STEVE NYERERE APATA PIGO.

Msanii wa maigizo na mchekeshaji mkongwe kutoka Bongo Movie Steve Mengele maarufu kama Steve Nyerere amepata pigo la kufiwa na mtoto wake leo hii maeneo ya kinondoni, kwa sasa Steve yupo kwenye ziara ya Tamasha la  Serengeti fiesta 2012.



CLOUDS MEDIA NA WASANII WA BONGO FLEVA NA BONGO MOVIES WATOA MSAADA DODOMA

Picha ya pamoja ya uongozi wa Clouds Media na Wasanii wa Bongo Fleva na Wasanii wa Bongo movies wakiwa pamoja na Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini na watoto wa kituo cha The Village of Hope pamoja na walezi wao cha Mkoa wa Dodoma
Msanii Diamond akiwasalimia watoto wa kituo hicho pamoja na kuwaimbisha nyimbo zake
Father Vicent Boselli akitoa maelezo ya kituo hicho kwa wasanii na viongozi wa Clouds Media


Baadhi ya walezi wakiwa wamebeba watoto wa kituo hicho

Anti Ezekiel akijitambulisha huku akiwa amembeba mmoja ya watoto wanaolelewa na kituo hicho

Wasanii Juma Nature na Shettah wakisalimia watoto wa kituo hicho

Hapa wakikabidhi misaada mbalimbali


Baadhi ya wanafunzi wa kujitolea kutoka maeneo mbalimbali duniani wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo hicho

Misaada akiingizwa ndani



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU