Msafara maarufu kwa jina la "Annual Animal Migration" unaohusisha wanyama aina ya Nyumbu wakiwa wanarudi katika mbuga ya Serengeti ya Tanzania wakiwa wanatoka katika mbuga ya Masai mara ya Kenya. Nyumbu hao walisafiri umbali wa zaidi ya kilometa 1000 katika mapumziko yao hayo. Msafara huo ambao ni maarufu zaidi duniani umevuta watalii wengi. Mwaka huu Nyumbu hao wamewahi kurudi kutokana na mvua zilizowahi kunyesha nchini Tanzania ambazo zimewawekea mazingira mazuri ya chakula. Nyumbu hao hukutana na mikasa na mazingira magumu wakati wa safari yao hiyo ambapo huwabidi kukatiza katika mto ambao una mamba na viboko ambao nao huwafanya msosi. Nyumbu hao waliorudi wanakaribia kuwa zaidi ya milioni moja na laki tano na huu ni msafara wa awali.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog