Facebook Comments Box

Sunday, February 22, 2015

LEO NDIYO LEO FAINALI YA LIGI DARAJA LA KWANZA KATI YA MWADUI FC NA AFRICAN SPORTS YA TANGA NDANI YA AZAM COMPLEX CHAMAZI


Mwadui FC

African Sports

Fainali ya kumsaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL), inatarajiwa kufanyika leo kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi kuanzia majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Awali mchezo huo wa fainali ulikuwa umepangwa kufanyika leo kwenye dimba la Uwanja wa Taifa, lakini kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TTF imelazimika kuhamishia mchezo huo Chamazi.

Mchezo huo wa fainali utaanza saa 10 kamili jioni, na utaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Azam TV ili kuwapa nafasi wapenzi na wadau wa soka waliopo mbali na hasa mikoani kuweza kushuhudia mchezo huo.

Bingwa wa Fainali ya Ligi Daraja la Kwanza atazawadiwa Kombe pamoja na medali, huku mshindi wa pili akipata kikombe na medali pia. Viingilio vya mchezo huo ni tsh.5,000 kwa jukwaa kuu na tsh. 3,000 kwa majukwaa ya mzunguko.

Lakini pia katika uwanja huo wa Azam Cmplex kutakuwa na mpambano mwingine wa wenyeji Azam watakao cheza na Tanzania Prisons ambapo mchezo huo utaanza majira ya saa mbili kamili usiku.

Mjini Shinyanga wenyeji timu ya Stand United wataikaribisha Simba SC kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, huku wagonga nyundo wa jiji la Mbeya, timu ya Mbeya City wakicheza na timu ya Young Africans kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

 IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA

MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU