Nchi ya Uturuki imeondoa marufuku ya kuvaa Hijabu kwa wanafunzi wa shule za Sekondari iliyodumu takribani kwa muda wa muongo mmoja.
Uamuzi huo ulitangazwa siku ya Jumanne na Naibu Waziri Mkuu Bulent Arinc.
Akizungumza na waandishi wa habari Bulent Arinc alisema kwa sasa serikali imeruhusu wanafunzi kuhudhuria shuleni wakiwa wamevaa Hijabu katika shule zote zilizo chini ya Wizara ya
Elimu.
Bulent Arinc ambaye ni msemaji pia wa chama cha Justice and Development (AK) alisema agizo hilo baada ya siku mbili litakuwa lenye kutekelezwa baada ya kupeleka taarifa za kimaandishi katika Wizara husika.
Hijabu ilipigwa marufuku mwaka 1980 kwa wanafunzi, wafanyakazi katika taasisi za umma na serikali muda mfupi baada ya mapinduzi ya kijeshi.
Tangu wakati huo wanawake waliokuwa wakivaa hijabu nchini humo walilazimika kuacha kazi katika ofisi za serikali.
Utawala wa Uturuki umekuwa ukijaribu kuwa mbali na taratibu za kiislamu kwa ajili ya kuridhisha nchi za Ulaya ili kuingizwa katika
umoja wa nchi hizo. Uturuki kwa muda mrefu imetaka kuwa mwanachama wa nchi hizo
za Ulaya bila mafanikio.
umoja wa nchi hizo. Uturuki kwa muda mrefu imetaka kuwa mwanachama wa nchi hizo
za Ulaya bila mafanikio.
Waziri Mkuu ErdoÄŸan aliahidi kuondoa marufuku yote juu ya uvaaji wa Hijabu wakati aliposhinda kwa mara kwanza mwaka 2002.
Tangu wakati huo aliondoa marufuku ya kuvaa Hijabu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Hata hivyo bado vazi la Hijabu halijaruhusiwa kwa majaji, waendesha mashtaka, maafisa wa kijeshi na wafanyakazi wa kijeshi.
Cha kuzingatia ni kuwa katika baadhi ya nchi za ulaya ikiwemo uingereza vazi la hijjab linavaliwa na watu wote hata askari kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog