Hiyo ni sare ya pili mfululizo kwa kocha Mzambia, Patrick Phiri baada ya wiki iliyopita kutoka 2-2 na Coastal Union Uwanja wa Taifa, licha ya kuongoza 2-0 hadi mapumziko.
Hadi mapumziko, tayari Simba SC ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Mganda, Emmanuel Okwi dakika ya 32 akimalizia pasi fupi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
Timu ya Polisi inayofundishwa na Mohammed ‘Adoph’ Rishard ilibadilika na kuanza kusukuma mashambulizi langoni mwa Simba SC ambapo Danny Mrwanda, mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, aliisawazishia Polisi baada ya kumzidi mbio na maarifa beki Joseph Owino kabla ya kumchambua vizuri kipa Hussein Sharrif ‘Cassilas’.
Azam FC imepata ushindi wake wa pili baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting leo kwenye Uwanja wa Chamazi.
Azam FC ambao walianza ligi kwa kuitwanga Polisi Moro kwa mabao 3-1, imeshinda mabao hayo mawili leo, yote yakitupiwa kimiani na Mrundi, Didier Kavumbagu ambaye sasa ana mabao manne.
Azam FC 2 - 0 Ruvu Shooting
Mtibwa Sugar 3 – 1 Ndanda FC
Mbeya City 1 – 0 Coast Union
Mgambo Shooting 0 – 1 Stendi United
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog