Facebook Comments Box

Thursday, September 25, 2014

CHUO CHA IMTU CHAFUNGWA NA TCU

TUME ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) Imekifungia kwa mda,Chuo kikuu cha tiba na Sayansi IMTU kutofanya udahili kwa Wanafunzi wapya wa Mwaka wa Masomo 2014-2015,kutokana na chuo hicho kukiuka sheria ya inayosimamia Vyuo Vikuu nchini.

Uamuzi huo wa kikifungia Chuo hicho
Umetangazwa mda huu Jijini Dar Es Salaam na Kaimu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) Profesa Magishi N Mgasa wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari ambapo alisema maamuzi hayo yamefikiwa baada kikao cha Dharura kilichoitishwa na (TCU) wiki iliyopita na kujadili taarifa ya timu iliyotathimini chuo hicho, Ambapo kikao hicho kikabaini mapungufu makubwa katika chuo cha IMTU yakiwemo matatizo ya uongozi,kukosa wahadhiri wakutosha na wenye sifa,kutokuwepo na Vifaa pamoja na kudahili wanafunzi bila hata kuwa na taratibu zilizowekwa na tume.

Profesa Mgasa alisema kwa kufanya hivyo chuo cha IMTU imekiuka sheria ya namba 5(1),sura ya 346 ya sheria za Tanzania ambayo inakitaka chuo Kikuu chochote kufuata taratibu zilizowekwa na tume.
Vilevile Profesa Mgasa alizidi kusema baada ya Tume kubaini makosa hayo,ndipo wamefikia maamuzi ya kukifungia chuo cha IMTU kufanya
udahili kwa wanafunzi wapya wa Mwaka
2014-2015,mpaka pale itakakapo rekebisha mapungufu yaliyotajwa na Tcu.

Pia tume imetoa notsi ya miezi 3 kwa chuo cha IMTU,kuanzia tarehe 16 mwezi huu kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza na endapo chuo hicho kikikaidi basi TCU haitosita kuwachukulia hatua kali ikewemo hata kukifungia kabisa.
Aidha Profesa Mgasa aliwataka wanafunzi nchini wasijiunge na chuo Kikuu chochote bila ya kufuata maelekezo kutoka Tume ya vyuo Vikuu
nchini (TCU).


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU