Facebook Comments Box

Friday, October 24, 2014

Q.CHILLAH AELEZEA NANI MKALI KATI YA DIAMOND NA ALI KIBA

Msanii wa Bongo Fleva Q. Chillah

Mapya yanazidi kuibuka kuhusu ushindani wa Diamond na Ali Kiba ambapoushindani huo ulianzia katika hitimisho la tamasha la Fiesta lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club Dar. 

Mashabiki wa wasanii hawa wawili wanavutana huku kila mmoja akisema mwenzake ana kipaji na anamfunika mwenzake. Inasemekana kuwa kuna baadhi ya mashabiki walikodiwa kwa ajili ya kumzomea Diamond wakati akitoa burudani siku ya Fiesta na hilo lilithibitishwa na Babu Tale ambaye ni meneja wa Diamond.

kwa sasa katika mziki wa Bongo Flava kumekuwa na fitina nyingi wakati mwingine wasanii kwa wasanii wanachonganishwa na mwisho wa siku unakuwa ugomvi, kwa mfano sasa hivi bifu la Ali Kiba na Diamond.

Q Chief : "Yote wanayopitia ni changamoto ambazo pengine hawakuwahi kuzania kwamba watapitia. Mimi nimepitia situation ambazo zimenijenga kuwa "sugu" na "Legendary" ndiyo maana ya kuwa mkongwe unapitia situation ambazo watu wengine wanakulazimisha ufike huko. 

Hata kama upo level fulani wanakushusha kwa kufikiria kwamba wanaweza kukushusha. Unapandishwa na watu, unapandishwa na mwenyezi Mungu, unashushwa na watu, unashushwa na mwenyezi Mungu. 

Mfano niliangalia Fiesta kwenye TV sikwenda kwa sababu nilikuwa na mambo yangu Studio, hakuna kitu kigeni nlichokiona, nimeona msanii wa marekani anafunikwa na msanii wa Tanzania ambaye ni Ali Kiba. 

Nmeona Ali Kiba ambaye amekaa kimya kwa miaka mitatu bila Airtime na watu wamemzungumzia vibaya, vizuri na nini wamemkubali tena. Ikiwa ni mtu yule yule ambaye wamemkataa na wakumuweka mtu mwingine juu. 

Hakuna kitu kisichowezekana, matokeo uliyoyaona juzi ndio matokeo yanayotokea na yataendelea kutokea. Hakuna Mungu wa hii kazi, hakunaga mfalme wa hii kazi ila kuna masultan wa Hii Kazi.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU