Facebook Comments Box

Friday, October 24, 2014

HATIMAYE DIAMOND ASALIMISHA SARE ZA JESHI

Kushoto ni Ney wamitego, Diamond Platnum, na Dancer wa Diamond wakiwa katika jukwaa la Fiesta hivi karibuni wakiwa wamevalia mavazi ya Jeshi.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond', amekiri kuhojiwa na polisi baada ya kukutwa na hatia ya kuvaa mavazi yanayoaminika kuwa ni sare ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Hata hivyo msanii huyo alidai kwamba mavazi hayo hayakuwa sare za jeshi hilo na kwamba yeye aliyanunua alipokuwa Ujerumani ingawa baada ya kuhojiwa aliyasalimisha.

Diamond alipanda jukwaani Jumamosi iliyopita katika onyesho la Fiesta jijini Dar es Salaam akiwa na mavazi hayo jambo ambalo liliibua mjadala kwa watu walio wengi.

Diamond alikiri kupata ujumbe uliomtaka kufika Kituo cha Oysterbay, Dar es Salaam na madansa wake akiwa na nguo hizo,
"Awali Meneja wangu alishikiliwa kwa muda na mimi nikatakiwa kufika na zile nguo nikiwa na madansa wangu ambao pia walizivaa, nilifanya hivyo na kuziacha nguo baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika," alisema.

"Nisingeweza kukaidi amri ya dola, nilifika na yale mavazi na nikahojiwa kwa saa kadhaa. Nikaeleza kwamba yalikuwa yakifanana tu na ya jeshi na hayakuwa sare rasmi za jeshi, kikubwa nilihitaji kumaliza tatizo," alisema.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU