Wakiwa ni wenye matumaini makubwa Yanga waliosindikizwa na mashabiki lukuki walijikuta wakikubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wakata miwa wa Turiani Mtibwa Sugar inayonolewa na kocha Mecky Mexime.
Mabao ya Mtibwa katika mchezo huo uliokuwa wa kasi kwa dakika zote 90 yaliwekwa kimiani na mshambuliaji wa zamani wa Simba na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mussa Hassan 'Mgosi' kwenye dakika ya 15 wakati msumari wa pili ukishindiliwa kimiani na Ali Ame kwenye dakika ya 83.
Katika mtanange huo pia ulishudia mshambuliaji pendwa katika kikosi cha Yanga Geilson Santos Jaja akikosa penati kwenye dakika ya 46 ya kipindi cha pili cha mchezo iliyopanguliwa na kipa wa Mtibwa Said Mohammed.
Yanga walionekana kuutawala mchezo huo kwa kipindi kirefu lakini Mtibwa walionekana kunufaika zaidi na mipira ya 'counter Attack' mashambulizi ya kushtukiza yaliowapa mabao yao mawili kwa njia nyepesi.
KIKOSI CHA YANGA KILIWAKILISHWA NA
1. Deo Munish "Dida" - 30
2. Juma Abdul - 12
3. Oscar Joshua - 3
4. Nadir Haroub "Cannavaro" - 23
5. Kelvin Yondani - 5
6. Mbuyu Twite - 6
7. Hassan Dilunga - 26
8. Haruna Niyonzima - 8
9. Geillson Santana "Jaja" - 9
10. Mrisho Ngasa - 17
11. Hamis Kizza - 20
Subs:
1. Juma Kaseja - 13
2. Rajab Zahir - 4
3. Omega Seme - 14
4. Nizar Khalfani - 16
5. Saimon Msuva - 27
6. Hussein Javu - 21
7. Said Bahanuzi - 11
1. Juma Kaseja - 13
2. Rajab Zahir - 4
3. Omega Seme - 14
4. Nizar Khalfani - 16
5. Saimon Msuva - 27
6. Hussein Javu - 21
7. Said Bahanuzi - 11
YANGA WAKIPASHA KABLA YA MCHEZO KUANZA |
MASHABIKI WA YANGA WAKIFATILIA KWA MAKINI MCHEZO |
YANGA WAKIPASHA |
BASI LA MASHABIKI WA YANGA KUTOKA DAR-ES-SALAAM |
YANGA WAKITOKA UWANJANI CHINI YA ULINZI MKALI |
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog