Samaki aina ya Goldfish, anaendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji kutolewa uvimbe kwenye ubongo wake. Upasuaji huo umesemekana kufanywa kwa uangalifu
mkubwa kutokana na hofu yatisho kwa maisha ya Samaki huyo. Samaki huyo kwa jina George, ambaye mmiliki wake anaishi Melbourne, alidunguwa sindano ya kuondoa fahamu iliyogharimu dola 200.
Wataalamu wa matibabu ya wanyama, wanasema kuwa Samaki huyo mwenye umri wa miaka 10, anatarajiwa kuiishi kwa miaka mingine 20.
"George
alikuwa na uvimbe mkubwa sana kwenye ubongo wake na alikuwa anakuwa
polepole sana, na hali hiyo ilikuwa inaanza kuathiri maisha yake,''
alisema daktari Rich kutoka hospitali ya matibabu kwa wanyama ya Lort
Smith. Mmiliki wa George, alikuwa ameambiwa achague kati ya Samaki huyo kufanyiwa upasuaji au adungwe sindano ya kulala.
Lakini aliona bora kujaribu kuokoa maisha ya Samakai wake na ndipo akakubali Samaki huyo afanyiwe upasuaji. Aliongeza kuwa Samaki huyo alisalia kuwa hai kutokana na madaktari kuweka hewa ya Oxygen kwenye maji wakati wa upasuaji
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog