Hali
katika klabu ya
Yanga kwa upande wa
walinda milango inaonekana
si shwari, hali hiyo ilijionyesha
dhahiri wakati wa
mchezo wa ngao
ya jamii ambao
pia ni maalumu
kama mchezo wa
ufunguzi wa pazia ya ligi
kuu ya Tanzania
al maarufu Vodacom
Premier Leagu (VPL). wakati
timu hiyo ya wana
Jangwani walikuwa wakimbana
na timu ya waoka mikate Azam Fc
(wana lamba lamba.)
Kilichowashtua
wengi ni kule kutokuwepo
kwa ushirikiano hata
kidogo kwa walinda milango hao
kabla ya mchezo huo
kuanza, kwa kawaida wakati
timu inayoanza huwa inachukuliwa
na mwalimu msaidizi
kwa ajili ya kuwapa
mazoezi ya kupasha
misuli joto makipa
huwa wanakuwa na
mwalimu wao huku akiwafanyisha
mazoezi kabla ya
mchezo, hivyo ndivyo
hali ndiyo ilivyokuwa
kwa upande wa
Azam wakati wachezaji
waliokuwa wanatarajiwa kuanza
walikuwa na Trainer (mkufunzi) wao Ibrahim
Shikanda mchezaji wao wa
zamani wale wa
akiba wao walikuwa
na mwl Kally
Ongara akiwapasha joto kwa
kufanya nao mazoezi
mepesi mepesi, kwa upande
wa makipa wao
walikuwa na mwalimu
wao Idd Abubakar
‘Phantom’ aliyekuwa akiwafanyisha
mazoezi ya kwa pamoja
huku wakishirikiana na
hata walipomaliza walikusanyika
wao watatu mwalimu
Idd Abubakar, Mwadini Ally
na Ayishi Manula
kwa pamoja wakaomba
dua bila kujali
nani anaanza katika
mchezo huo ndiyo
wakaenda ndani kwenye
vyumba vyao vya
kubadilishia nguo.
Kwa
upande wa yanga
wao wale wanaonza
walikuwa na mwalimu
Salvatory Edward na Mwalimu
wao Mbrazil
Leiva,wale wasioaanza kwenye mchezo
ule wao walikuwa
wakisimamiwa na mwalimu
Shedrack Nsajigwa "FUSO" huku
wakifanya mazoezi mepesi.
Kazi ilikuwa kwa walinda mlango wao sasa ndiyo walioonekana hawakuwa na ushirikiano hata kidogo kuanzia walipoingia, Dida alikuwa mbele ya wachezaji wakati Kaseja yeye alikuwa yuko nyuma ya wachezaji wengine na hakuna sehemu yoyote ambayo walishirikiana hata mmoja kumpa mwenzake mpira kitu ambacho si cha kawaida kwa walinda milango na aina ya mazoezi wanayoyafanya kabla ya kuanza kwa mchezo hicho ni kitu cha kwanza.
Kitu cha pili, hata mwalimu wao Pondamali yeye hakujishughulisha na kumuandaa Kaseja pia kwa ajili ya mchezo huku akijua kwamba hata dakika ya 10 tu ya mchezo Dida akiumia atayeiingia ni Kaseja ambaye yeye alikuwa hajishughulishi kabisa na kumuandaa kimchezo hali ambayo ilizusha maswali kwa wale baadhi tu tuliogundua kitu hicho na baadhi yetu tukawa tunakwama yupi yuko sahihi kwa kuwaandaa makipa kwa kile kilichokuwa kinaendelea pale uwanjani kati ya mwalimu Pondamali wa Yanga na mwalimu Idd Abubakar wa Azam bila kupata majibu.
kitu cha tatu na cha mwisho ambacho ni pale Kaseja alipojitenga kabisa na Pondamali na Dida.

wakati wao wakiendelea
na mazoezi yeye
alikuwa pembeni kabisa
akicheza ule mchezo
maarufu sana dana
dana huku akifanya
manjonjo ya kuuchezea
mpira peke yake
mpaka alipopata msaidizi
na yeye kwa
kuwa anapigiwa mpira
na mtu wa
vifaa wa Yanga.
Hii
si kawaida kitimu
na haijawahi kutokea
kwenye timu yeyote
walipokuwa pamoja kuanzia
Simba na hata
Timu ya Taifa Stars
na hata pale
Kaseja alipokuwa na
Ivo Mpaunda Timu
ya taifa haijawahi
kujitokeza hali ya
namna hii kiasi
cha wadau pia
kuona kuwa Pondamali
pia ni chanzo cha kuwagawa makipa
hao kwa kuwa
yeye kama mwalimu
wao haonyeshi jitihada
za kutaka kuonyesha
kuwe na ushirikiano pale wanapokuwa
kwenye mechi kama
ilivyokuwa katika mchezo
huo wa ngao.
Ndiyo maana kitongoni inahisi kuwa kuna siri nzito ndani ya Yanga inayowahusisha Juma Kaseja, Deo Munishi Dida, mwalimu wao Juma Pondamali Mensah na huenda hata Benchi zima la ufundi chini ya Mbrazil Maxio Maximo wanajua nini kinaendelea katika wawili hao na jitihada zetu za kuzitafuta pande zote 3 zinaendelea.

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog