Katika mechi hizo zilizofanyika jumapili jioni na usiku Yanga iliteremka dimbani kupambana na Shangani fc inayoshiriki daraja la pili wilaya ya mjini hapa unguja na Simba ikapambana na Kilimani City nayo pia inashiriki katika daraja hilo hilo la pili wilya ya mjini, katika pambano la kwanza la Yanga liliofanyika majira ya saa 10 jioni liliingiza shilingi mil 7.3, wakati lile la pili liloanza majira ya saa 2 usiku lilioihusisha timu ya Simba liliingiza shilingi mil 3.1 tu na kuzusha maswali mengi sana kwa wadau.
kwa kuwa pambano hilo lililofanyika usiku na kuhudhuriwa na watu wengi sana kuliko wale wa mchana,hali hiyo ilifanya viongozi wa Simba wa mjini hapa wakiongozwa na Bw. Abdul Mshangama kuhoji kulikoni wao wapate mapato kiduchu namna hiyo na wakati kwenye mechi yao ndiyo kulikuwa na watu wengi na wamewatupia lawama kuwa Kilimani City wamechakachua mapato hayo.
Viongozi wa Mlimani walipatwa na kigugumizi na kuonyesha kusikistishwa na hilo licha ya viongozi hao kuomba radhi. Hali iliyosababisha hasira za viongozi wa Simba na kuwaambia wao walikuwa wamejenga urafiki lakini wameonyesha si waminifu katika pesa hizo ndogo
"hizo pesa ni ndogo na kusema kuwa kama wao Kilimani ndiyo waliomba na kuna makubaliano walikubaliana juu ya usimamizi na mgawanyo wa mechi mapato hayo na hata kama watataka waje Dar tutacheza nao na hata kama wanahitaji msaada wa kipesa tutawapa bila shida ila hawakutufurahisha kwa kweli" alisema kiongozi mmoja wa simba
Nayo ZFA wilaya ya mjini kupitia katibu wake Yahya Juma Ally wameshngazwa na tukio hilo huku wakiwatupia lawama viongozi hao wa Kilimani
"kwa kuwa waliwaambia viongozi wa Kilimani City walete vitabu vyote vya tiketi ili vigongwe muhuri wa ZFA na baadae sisi tuje kusimamia hata milangoni lakini wenzetu walienda kinyume wakaleta vitabu kidogo tu na hata milangoni wakawa wao wenyewe bila kuishirikisha ZFA" alisema kiongozi wa ZFA
Kwa hili lililotokea ZFA wilaya mjini tumesikitishwa sana na fedheha hii tuliyopewa na timu ya kilimani City na tutajitahidi lisitokee tena kwenye mechi zijazo aliongeza kiongozi huyo wa ZFA.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog