“ Nao hawakuona baya lolote kwao ila tu kwa kuwa wamemuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa ” (TMQ 85:8)
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki inalaani kwa nguvu zote mateso, unyama, udhalilishaji na ushenzi mkubwa wanayofanyiwa ndugu zetu Waislamu wakiwemo masheikh, maustadh na wanaharakati wa Kiislamu walioko katika kesi inayodaiwa ya ugaidi, kama walivyoeleza wenyewe karibuni mahkamani jijini Dar es-Salaam na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Sisi katikaHizb tunaweka bayana kwamba: mateso, unyama, ukatili na ushenzi wanaotendewa ndugu zetu Waislamu hao na wengineo ni kwa sababu tu ya Uislamu wao na si vyenginevyo. Kwa sababu kimsingi sheria ya kibaguzi inayoitwa ya ‘ugaidi’ imelazimishwa na
Marekani kwa ajili ya kuwadhulumia Waislamu. Hizb inauliza kwa kinywa kipana pale viongozi wa kanisa akiwemo Mchungaji Mtikila ambaye mara kwa mara huwekwa korokoroni, kuhojiwa na
Polisi hadi kufungwa jela. Jee kuna siku yoyote aliwahi kufanyiwa ushenzi, mateso na unyama kama wanaofanyiwa ndugu zetu hao Waislamu ?
Tunasema tena, vitendo hivi vya mateso na dhulma ambavyo hufanyiwa Waislamu na vikosi maalumu kwa agizo la Marekani sio mwanzo Tanzania wala sio mwisho. Bali vimeenea duniani kote kuanzia katika kambi za mateso za Marekani za Guntanamo, Balgram, Abu Ghuraib nk.
Aidha, mateso yaliyotajwa mahkamani hapo na Waislamu hao ni machache kuliko halihalisi ilivyo. Hususan kwa ndugu zetu waliobambikiziwa kesi kama hizo wakiwemo Waislamu wenzetu wa Arusha, Mwanza, Kenya nk.
Mateso haya hutendwa kupitia vikosi maalum vinavyosimamiwa na Marekani vinavyoitwa ati vya kupambana na ugaidi ambavyo licha ya kukosolewa, kukashifiwa, kufedhehewa na kulaumiwa vikali hadharani kwa uovu wao kama ilivyofunua taarifa ya tarehe 18/08/2014 ya Mashirika ya Utetezi la Haki za binadamu kwa
kikosi cha ATPU cha kupambana ugaidi nchini Kenya.
Aidha, mateso yaliyotajwa mahkamani hapo na Waislamu hao ni machache kuliko halihalisi ilivyo. Hususan kwa ndugu zetu waliobambikiziwa kesi kama hizo wakiwemo Waislamu wenzetu wa Arusha, Mwanza, Kenya nk.
Mateso haya hutendwa kupitia vikosi maalum vinavyosimamiwa na Marekani vinavyoitwa ati vya kupambana na ugaidi ambavyo licha ya kukosolewa, kukashifiwa, kufedhehewa na kulaumiwa vikali hadharani kwa uovu wao kama ilivyofunua taarifa ya tarehe 18/08/2014 ya Mashirika ya Utetezi la Haki za binadamu kwa
kikosi cha ATPU cha kupambana ugaidi nchini Kenya.
Pamoja na fedheha hizo za hadharani kutoka kwa taasisi zao wenyewe, bado vikosi hivi vinaonekana kujigubika uziwi na kuendeleza maovu, dhulma, mateso na udhalilishaji wa wazi kwa Waislamu.
Vitendo hivi ni miongoni mwa dalili nyingi za kudhihirisha udhaifu na fedheha kubwa kwa mfumo wa kibepari. Kwanza, kutokuwa na muundombinu thabiti wa ukusanyaji ushahidi, kama kuna ushahidi kamwe katika kesi na badala yake kutegemea utesaji. Pili, dhihirisho la kukosekana uzito shauri/ kesi husika kiasi cha vikosi hivi kumalizia chuki na ghadhabu zao kwa
watuhumiwa kwa kuwatesa. Kwa kuwa wana yakini hakuna kesi itakayoendelea. Tatu, dhana ya kitoto na ndoto za mchana za bwana wao Marekani na mfumo wake wa wa kikafiri wa kibepari kudhani ati kuwatesa Waislamu kutawatisha Umma wa Kiislamu waache na waogope uwajibu wao wa kuhubiri na kutangaza dinibyao ya haki.
Marekani na vikosi vyake vinavyoitwa vya kupambana na ugaidi wanaelea katika ndoto za mchana na kugubikwa na ujinga wa kutojua historia wakidhani kuwa Uislamu utamalizika
kwa kuteswa Waislamu. Lau ingekuwa ndoto yao hiyo ndio uhalisia, basi Uislamu leo usingetajwa kamwe katika uso wa ulimwengu.
kwa kuteswa Waislamu. Lau ingekuwa ndoto yao hiyo ndio uhalisia, basi Uislamu leo usingetajwa kamwe katika uso wa ulimwengu.
Na nne, ni kushindwa watetezi wa mfumo wa kibepari kutetea mfumo wao kwa hoja na dalili. Badala yake katika kutapatapa na khofu ya kumalizika mfumo wao huwa hawana namna ila kutesa Waislamu. Kwa kuwa kimaumbile ubepari
hauwezi na hautoweza kujitetea kwa hoja za kidini wala za kiakili.
hauwezi na hautoweza kujitetea kwa hoja za kidini wala za kiakili.
Kimsingi umezaliwa kwa ajili ya kufa! Na punde InshaaAllah utatupwa katika jalala la kihistoria. Kwa kuwa hauna manufaa kwa ubinaadamu zaidi ya madhila na kushindwa juu ya kushindwa.
Umeshindwa ubepari katika siasa ukidai kuna demokrasia kumbe ni nidhamu ya udanganyifu na matajiri. Hudai katiba itokane na watu kumbe tayari wana katiba yao mfukoni, umeshindwa
kiuchumi kwa kuongeza msururu wa makodi na umasikini, huku makampuni ya kibepari yakipora rasilmali kwa baraka za wanasiasa waovu na mikataba ya udanganyifu, umeshindwa katika upande wa kijamii kwa kupitia fikra chafu za
‘uhuru’ (freedoms) kwa kuongeza maovu na mabalaa mbali mbali kwa mwanadamu kuanzia ulevi, zinaa, kupigia debe vitendo viovu vya ushoga, usagaji nk.
Na vitendo hivi vya utesaji na udhalilishaji Waislamu katika mchakato wa kisheria ni kushindwa kuliko dhahiri kukosekana kinachoitwa utawala wa sheria na udhaifu katika taasisi za mahkama za kusimimia haki na sheria. Ajabu na aibu kubwa!
wanashindwa hata kusimamia sheria walizozitunga kwa mikono yao ! Basi nini cha kutarajia kutoka mfumo huu zaidi ya damu na
machozi !
Baada ya yote hayo Hizb inawasisitiza Waislamu kuendelea kuulingania Uislamu wao bila ya khofu wala woga kwa njia ya Mtume SAAW ambayo haihusishi utumiaji wa nguvu wala
mabavu. Pia wafedhehi kila aina ya vitendo vya dhulma wanavyotendewa Waislamu, na kuachana na michakato yote ya siasa za kikafiri za kidemokrasia , zikiwemo katiba zake na
chaguzi zake. Kwa kuwa ni haramu na zaidi ndio zinazodhamini kupatikana watawala wanaosaidia kudhuru Waislamu.
mabavu. Pia wafedhehi kila aina ya vitendo vya dhulma wanavyotendewa Waislamu, na kuachana na michakato yote ya siasa za kikafiri za kidemokrasia , zikiwemo katiba zake na
chaguzi zake. Kwa kuwa ni haramu na zaidi ndio zinazodhamini kupatikana watawala wanaosaidia kudhuru Waislamu.
Aidha, tunawafariji ndugu zetu na Waislamu jumla kwa madhila haya na mengineyo. Lakini pia tunawapa Waislamu bishara ya ushindi wa Umma wetu chini ya kivuli cha dola tukufu ya Kiislamu ya Pili ya Khilafah Rashidah. Dola hiyo haitosahau dhulma hata yenye ukubwa wa punje ya hardali aliyotendewa Muislamu ila itamhukumu dhalimu. Na lau madhaalimu wataondoka duniani kabla ya kurejea dola hiyo. Pia hawatosalimika wala kunusurika na adhabu ya Muumba ambae kamwe hajawasahau, hasahau wala hatosahau na dhulma yao.
﴿ ﻭَﻻَ ﺗَﺤْﺴَﺒَﻦَّ ﺍﻟﻠَّﻪَ ﻏَﺎﻓِﻼً ﻋَﻤَّﺎ ﻳَﻌْﻤَﻞُ ﺍﻟﻈَّﺎﻟِﻤُﻮﻥَ ﺇِﻧَّﻤَﺎ ﻳُﺆَﺧِّﺮُﻫُﻢْ ﻟِﻴَﻮْﻡٍ
ﺗَﺸْﺨَﺺُ ﻓِﻴﻪِ ﺍﻷَﺑْﺼَﺎﺭُ ﴾
“ Na wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na yale watendayo madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatakapokodoka macho yao .” (TMQ 14: 42
Masoud Msellem
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb-ut Tahrir Afrika Mashariki
Kumb: 21 / 1435 AH jumaa, 26th Shawwal 1435 AH
22/08/2014 CE
Tel +255 778 870609
Pepe: jukwalakhilafah@gmail.com
Tovuti Rasmi ya Hizb ut- Tahrir
www.hizb-ut-tahrir.org
Tovuti ya Afisi ya Habari
www.hizb-ut-tahrir.info
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb-ut Tahrir Afrika Mashariki
Kumb: 21 / 1435 AH jumaa, 26th Shawwal 1435 AH
22/08/2014 CE
Tel +255 778 870609
Pepe: jukwalakhilafah@gmail.com
Tovuti Rasmi ya Hizb ut- Tahrir
www.hizb-ut-tahrir.org
Tovuti ya Afisi ya Habari
www.hizb-ut-tahrir.info
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog