Facebook Comments Box

Wednesday, August 20, 2014

YANGA NA COASTAL ZAGONGANA PEMBA


Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Coast Union
Picha Maktaba:
 
Katika kile kilichodaiwa kuwa ni maandalizi ya Ligi kuu ya Tanzania Bara ambayo inataraji kuanza hapo mwezi ujao wa Tisa ilitokea hali ya kushangaza pale timu mbili ambazo pia zinajiandaa na ligi hiyo YANGA na COASTAL Ziligongana Pemba jana. 

Baada ya timu ya Yanga kutua kisiwani kwa mafungu (juzi)siku ya Jumatatu na timu ya Coastal union nayo ilitua kwa mafungu kisiwani humo jana (siku ya Jumanne). 

Hali hiyo ilileta mkanganyiko wa nani atautumia uwanja wa Gombani kabla ya kukubaliana kuwa timu zote zitakuwa na vipindi viwili vya kufanya maoezi uwanjani hapo ambapo Coastal ndiyo wanaanza saa 12 asubuhi mpaka saa 2 mbili asubuhi na Yanga wanaanza saa 2 asubuhi mpaka saa 4, na wanarudi tena saa 8 mchana mpaka saa 10 jioni, ndiyo Coastal wanaingia tena kumalizia awamu yao ya pili.

Awali iliarifiwa kuwa ziara ya wana jangwani hao ilipangwa kuanza tarehe za mwanzoni mwa mwezi huu hivyo kufikia tarehe 17 hadi 18 ndiyo wangekuwa wanaondoka, lakini kwa kuwa jambo hilo limewekwa sawa ratiba ndiyo itakuwa hiyo, kufatia timu 2 hizo za bara kugongana kisiwani humo na wekundu wa msimbazi kuwa Unguja wadau wanahoji kuna ni visiwani??

 Chanzo: kitongoni(Pemba)


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU