Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia.
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ametangaza amri ya kutotoka nje kwa wananchi wake nyakati za usiku kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi katika eneo la Kitongoji cha West Point viungani mwa Jiji la Monrovia.
Hali hiyo imetokana na tukio lililotokea hivi karibuni la watu kushambulia kituo cha afya katika eneo hilo na kusababisha wagonjwa 17 wa Ebola kutoroka.
Mgonjwa mmoja kati ya 17 waliotoroka katika kituo cha afya akiwa amebebwa na kijana.
Rais Sirleaf ameilaumu serikali yake kwa kutothibiti homa hiyo ya
Ebola, kwani haikufanya vya kutosha kuboresha hali ya maisha ya raia
walipopuuza ushauri wa wafanyakazi wa huduma za afya na kutotilia
maanani tahadhari rasmi za Ebola.
Hata baada ya Liberia kutangaza hali ya dharura
kufuatia mlipuko wa Ebola mapema mwezi huu, ugonjwa huo unazidi
kusababisha vifo nchini humo.
Ebola haina tiba lakini Shirika la Afya Duniani
(WHO) liliidhinisha matumizi ya dawa zilizokuwa zikifanyiwa utafiti
kufuatia mlipuko mkubwa wa Ebola Afrika Magharibi .
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog