Facebook Comments Box

Sunday, August 31, 2014

WAZIRI MKUU AKIMBILIA AFRIKA YA KUSINI

Jeshi la Lesotho
Sawa Waziri mkuu nchini Lesotho Tom Thabane ameiambia BBC kwamba amelitoroka taifa hilo baada ya kupata vitisho vya maisha yake.

Akizungumza kutoka nchini Afrika kusini,Bwana Thabane amesema kuwa vitendo vya jeshi nchini humo vya kusitisha huduma za serikali na kusababisha mapinduzi.
 
Awali Ripoti kutoka mji mkuu wa maseru zilisema kuwa jeshi lilizingira makao makuu ya polisi na kuzuia matangazo ya radio pamoja na mtandao wa simu katika mji mkuu wa Maseru.

Uchaguzi uliozongwa na utata nchini humo miaka miwili iliopita ulisababisha kuundwa kwa serikali ya muungano isio dhabiti.
Licha ya mazungumzo ya kuleta amani mnamo mwezi Juni ,hali ya wasiwasi ilitanda huku majirani wa taifa hiilo wakionya dhidi ya
mbinu yoyote isio ya kikatiba.
 
Taifa hilo limezungukwa na Afrika kusini na hutegemea sana jirani yake kwa maslahi pamoja na nafasi za kazi.

Chanzo: BBC SWAHILI


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU