Facebook Comments Box

Sunday, August 31, 2014

SIMBA YAVUNA MAGOLI KWA KMKM

Beki wa Simba "baba ubaya" akipambana na mchezaji wa KMKM
SIMBA SC imewafunga mabingwa wa Zanzibar, KMKM mabao 5 - 0 katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara usiku huu uwanja wa Amaan,Zanzibar.

KMKM inayofundishwa na Ally Bushiri ‘Bush’ ambayo Jumatano wiki hii ilifungwa 2 - 0 na Yanga SC, leo iligeuzwa asusa na Wekundu wa Msimbazi.

Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza mabao 4-0, yaliyotiwa kimiani na Hamis Tambwe mawili, Amir Kiembe na Shabaan Kisiga 'malone' moja kila mmoja.

Viongozi wa Simba wakiongozwa na Hans pope
Amri Kiemba ndiye aliyefungua karamu ya mabao ya Simba SC hii leo, dakika ya tatu ya mchezo baada ya kupewa pasi nzuri na kiungo Mrundi, Pierre Kwizera na kuwatoka wachezaji wawili wa KMKM kabla ya kufumua shuti kali lililogonga mwamba wa ndani wa lango.

Amisi Tambwe akafuatia dakika ya 14 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Salim Amour kufuatia yeye mwenyewe kupiga mkwaju wa penati, baada ya Kiungo Haroun Chanongo kuangushwa kwenye boksi.

Tambwe tena akafunga bao la tatu dakika ya 23 akimalizia krosi maridadi ya Ramadhan Singano 'Messi' kabla ya kisiga kufunga la nne dakika ya 37, kufuatia kazi nzuri ya Kiemba.

Mchezaji ambae yupo katika mgogoro na ambae hajajua hatma yake kama atacheza au hata cheza ligi Emmanuel Okwi akiwa katika benchi la simba akiangalia kama anaweza kupata namba katika kikosi hicho cha Simba.
Kipindi ha pili, kocha Mzambia, Patrick Phiri alibadilisha kikosi kizima akimuacha Nahodha Joseph Owino na dakika ya 60 Elias Maguri akahitimisha karamu ya mabao kwa bao safi la tano.

Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyetangaza juzi kurejea Simba SC kutoka kwa mahasimu wao Yanga SC usiku wa jana alikuwepo, lakini alibaki benchi muda wote wa mchezo.

Hamis Tambwe na Singano wakishangilia Goli
Viongozi wa Simba SC wakiongozwa Makamu wa
Rais, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na Mwenyekiti
Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe, Kassim
Dewji, Musley Ruwey, Mohammed Nassor ‘Steven
Seagal’, Crescentius Magori, Said Tuliy na
wengineo walikuwepo kushuhudia mchezo huo.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa:
Ivo Mapunda/
Hussein Sharrif ‘Cassilas’ dk46/Peter Manyika
dk84, Miraj Adam/Abdi Banda dk46/Nassor
Mssoud ‘Cholo’dk84, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’/
William Lucian ‘Gallas’ dk46/Mohammed Hussein
‘Tshabalala’ dk84, Joram Mgeveke/Hassan Isihaka
dk46, Joseph Owino, Pierre Kwizera/Abdallah
Seseme dk46, Haroun Chanongo/Twaha Ibrahim
‘Messi’ dk46, Amri Kiemba/Ibrahim Hajibu dk46,
Amisi Tambwe/Elias Maguri dk46, Shaaban Kisiga
‘Malone’/Awadh Juma dk46 na Ramadhani Singano
‘Messi’/Uhuru Suleiman dk46.
KMKM; Salim Amour, Pandu Hajji, Faki Hamad/
Makame Hajji dk30, Juma Rashid/Nassor Ali dk30,
Halfan Khamisi/Mudrik Muhibu dk30, Moka
Shaaban, Ame Khamis, Abdi Kassim ‘Babbi’, Haji
Simba/Kassim Nemshi dk30, Maulid Ibrahim na
Khamis Ali.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU