Meneja
Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Mkoa wa Ilala, Catherine Nkelebe
(kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana ,
kuhusu TRA mkoa huo kukamata bidhaa mbalimbali za dukani ambazo
wafanyabiashara wanadaiwa kukwepa kuzilipia kodi kupitia mashine za
kielektroniki.
Marobota ya bidhaa mbalimbali yakiwa TRA Mkoa wa Ilala baada ya kukamatwa.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA),
Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, imekamata bidhaa mbalimbali za
dukani zenye thamani ya mamilioni ya fedha ambazo wafanyabiashara
wamefanya hujuma ya kukwepa kulipa kodi kupitia mashine za
kielektroniki (EFD-Electronic Data Enterchange).
Meneja Msaidi wa TRA Ilala,
Catherin Nkelebe akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam, alisema bidhaa hizo ambazo ni pamoja na sufuria, Khanga na
mitumba zilikamatwa kufuatia msako unaoendeshwa na mamlaka hiyo kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Nkelebe alisema wafanyabishara
wamekuwa wakitumia mbinu nyingi kuwepa kulipa kodi kwa kukataa kutumia
mashine maalum za kielektroniki zilizotolewa na TRA kwa kukata
stakabadhi kwa wateja wanaokwenda kununua bidhaa katika maduka yao.
Alisema ujanja unaofanywa na
wafanyabiashara ni kwamba mteja akienda kununua bidhaa hususan katika
maduka ya jumla wanampatia stakabadhi yenye thamani ndogo wakati mzigo
huo unakuwa na thamani kubwa.
“Unakuta mfano mteja amenunua
bidhaa za thamani ya shilingi milioni moja lakini mwenye duka anampatia
stakabadhi mnunuaji yenye thamani ya Sh. 200,000 ili kukwepa kulipa
kodi,”alisema.
Nkelebe alisema hujuma nyingine
inayofanywa na wafanyabiashara ni kutoa stakabadhi ambazo hazina maelezo
yeyote au mchanganuo wa bidhaa zilizonunuliwa kwa lengo la kuiibia
serikali mapato yake.
Aliongeza kuwa wafanyabishara
wanafanya ujanja huo kwa hofu ya kwamba iwapo wataandika stakabadhi
yenye malipo halali watakadiliwa kiwango kikubwa cha kodi wakati siyo
kweli kwani TRA haifanya hivyo kwani inamkadiria mtu kodi kulingana na
biashara yake.
Alisema TRA kwa kushirikiana na
Jeshi la Polisi wataendelea kufanya msako wa wafanyabiashara wanaofanya
hujuma hizo na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog