RAIA wa Uingereza, Robert Dewar, amekamatwa na nyara za serikali zenye
thamani ya shilingi 118,314,900 jijini Dar es Salaam. Kamishna wa Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema mtuhumiwa huyo
ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trans Afrikas Logistics
(TALL), alikamatwa Agosti 9, 2013 saa mbili usuku huko Mbezi Beach,
Kinondoni akiwa na nyara hizo.
Alizitaja nyara hizo kuwa ni shanga mbalimbali zilizotengenezwa kwa meno ya tembo, vinyago 11, meno 20 na kucha 22 za Simba, ndege mmoja aina ya kasuku, vipande vya miti ya mpingo na idadi kubwa ya vinyago, vyote vikiwa na uzito wa kilogramu 24. Mtuhumiwa huyo pia alikutwa akiwa na mawe yanayodhaniwa kuwa ni madini pamoja na ganda moja la bomu.
Kamishna Kova aliongeza kuwa mtuhumiwa amekuwa akisafirisha vitu hivyo sehemu mbalimbali duniani, na kwamba atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika. --- Mwananchi na Tanzania Daima

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog