Facebook Comments Box

Friday, June 14, 2013

SERIKALI YAZIRUHUSU YANGA NA SIMBA KWENDA SUDAN


 
Kikosi cha mabingwa wa Tanzania na Afrika mashariki na kati (kagame cup) Yanga Sc
Kikosi cha washindi wa tatu wa Tanzania Simba Sc
 Siku moja baada ya Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuziteua timu za URA, Elite Sport ya Chard na Rayon Sports ya Rwanda kuziba nafasi za timu za Tanzania, Serikali jana imetangaza kuziruhusu timu hizo kushiriki michuano hiyo iliyopangwa kuanza Jumanne ijayo Juni 18 Durfur nchini Sudan.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Amosi Makalla alisema jana kuwa Serikali ya Sudan imewahakikishia kwa maandishi kuzipa usalama timu za Tanzania zitakazoenda kushiriki michuano hiyo ambayo Yanga ni bingwa mtetezi.

“Tulikuwa tunakataa kwa vile hatukupata taarifa rasmi ya maandishi kutoka serikali ya Sudan kutuhakikishia usalama wa watu wetu kuanzia uwanja wa ndege zitakapotua, zitakapokuwa Khatoum, ulinzi wa kuzitoa Khatorm hadi Durfur na hoteli watakazofikia, lakini jana imetuhakikishia usalama na siku zote Chama cha Soka cha Sudan ndio kilichokuwa kikituambia kuna usalama tusingeweza kuamini, lakini kwa vile tumepata udhibitisho wa serikali timu ruksa kwenda,” na kusisitiza: “Timu zote zilikuwa zinajiandaa na mashindano ni tarehe 18 kama zinataka kwenda ziende, na hao CECAFA kama wameteua timu nyingine iyo ni juu yao.”

Makala ambaye juzi alitoa msimamo wa serikali akipigilia nyundo kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje, Benard 
Membe alisema serikali ndio inajua hali ya usalama ya Durfur ilivyo hivyo haiwezi kuziruhusu timu za Simba, Yanga na Super Falcon ya Zanzibar zikashiriki michuan hiyo.

Hata hivyo viongozi wa Simba na Yanga jana walipoulizwa kuhusiana na suala hilo walionekana kuduwazwa kwani hawakuwa na taarifa yoyote ya serikali au TFF ikiwajulisha juu ya jambo hilo, huku timu zote zilishatoa msimamo wa kutoshiriki michuano hiyo baada ya kuambiwa Durfur si salama.

Laurance Mwalusako Katibu mkuu wa Yanga, “Hili suala kuna mgongano wa mambo mengi, mpaka sasa hivi klabu hatuna taarifa zozote, na isitoshe sisi jana tumevunja kambi na tumewapa wachezaji wetu mapumziko ya wiki mbili, hata hivyo tukipata tutakaa na kujadili kama tushiriki au la.”

Ismail Aden Rage Mwenyekiti Simba, “Mi sina habari zozote nipo na Waziri huku (Dodoma) mbona hajaniambia chochote, ngoja akishaniambia ndio tunaweza kutoa msimamo wetu lakini kwa sasa hatuna taarifa zozote.”

Hata hivyo licha ya serikali kuziruhusu hadi jana mchana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia kwa katibu wake Angetile Osiah alisema bado hawajapata taarifa rasmi zaidi ya taarifa ya juzi ambayo serikali waliituma kwa katibu wa CECAFA Nicholaus Musonye ya kutaka wadhibitishiwe kama kweli kuna usalama.

“Rais Tenga juzi aliwatumia barua ya Waziri wa Michezo wa Durfur ya kuwahakikisha usalama wa kutosha kwa timu zetu, zaidi ya hiyo hatujapata taarifa nyingine mpaka sasa hivi,” alisema Osiah.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU