Facebook Comments Box

Wednesday, September 18, 2013

MWIMBAJI WA ZANZIBAR NJEMA MODERN TAARAB PRINCE AHMED MGENI AFARIKI DUNIA




AHMED MGENI WAKATI WA UHAI WAKE KATIKA PICHA TOFAUTI JUU HAPO



MSANII wa muziki wa Taarab Prince Ahmed Mgeni amefariki dunia alfajiri ya leo Visiwani Zanzibar.

Mgeni alikutwa na umauti huo baada ya kuugua TB ya tumbo kwa muda mrefu anatarajiwa kuzikwa leo visiwani humo.

Enzi za uhai wake msanii huyo aliyepata kuimba katika bendi mbalimbali sambamba na kutoa nyimbo kadhaa zilizoteka alikutwa na umauti huo Alfajiri saa kumi ya kuamkia leo alipokuwa amelazwa katika hospitali ya Mnazi mmoja, Zanzibar.

Mwezi April mwaka huu 2013 mwimbaji huyo alizushiwa kifo baada ya hali yake kuwa mbaya

Moja ya kibao kilichompatia umarufu kilijulikana kama Sitetereki "Mlinzi wa kweli ni Mungu aso hiyana na mtu sio wewe mlimwengu hunibabaishi kitu.....

Mwili wa Msanii huyo umeishatolewa hospitali tayari kwa maziko saa kumi jioni leo nyumbani kwa Baba yake Amani Fresh - Zanzibar

'INNALILAHI WAINNAILAIHI RRAJIUN' 


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU