Facebook Comments Box

Tuesday, September 24, 2013

ETOILE DU SAHEL WAIOMBA SIMBA IMCHUKUE OKWI YAISHE JUU KWA JUU

Wakati straika Emmanuel Okwi akiwa Dar es Salaam, timu yake ya Etoile du Sahel imeendelea kufulia na kuitaka Simba imchukue mchezaji huyo ili mambo yaishe juu kwa juu.
Simba iliipa Etoile du Sahel mpaka Septemba 30 mwaka huu iwe imelipa Sh 480 milioni za kumnunua mchezaji huyo, lakini hilo halijafanyika mpaka sasa.
Wiki iliyopita, Simba iliandika barua kwenda kwa uongozi wa Etoile du Sahel, lakini timu hiyo ya Tunisia haijajibu lolote.“Jamaa wana hali mbaya kiuchumi, wanatulazimisha tumchukue Okwi, halafu watulipe fedha kidogo kama fidia, lakini bado sisi hatuafiki tunasubiri mpaka hiyo Septemba 30. 

Wakishindwa tunakwenda moja kwa moja Fifa,” alisema mmoja ya viongozi wa Simba jana Jumatatu.“Okwi mwenyewe yupo tayari kurudi Simba wakati wowote, lakini ngoja kwanza tusubiri hiyo Septemba 30 ambayo ndio siku ya mwisho tuliyokubaliana na Etoile du Sahel,” alisema.
Okwi mwenyewe ambaye yupo Dar es Salaam aliliambia Mwanaspoti jana Jumatatu kuwa amekuja nchini kwa mapumziko mafupi na kutuliza akili yake.


Katika mechi ya Jumamosi iliyopita, mashabiki walitaka kumvalisha Okwi jezi na skafu zenye nembo ya Simba, lakini alikataa kwani angekuwa anakwenda kinyume na mkataba wa Etoile du Sahel.
Okwi yupo nchini baada ya kualikwa na rafiki yake Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Simba, Abdulfatah Saleh, ambaye ndiye mmiliki wa hoteli ya Sapphire.
CHANZO:Mwanaspot


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU