Facebook Comments Box

Tuesday, July 30, 2013

UJUMBE ALIOPEWA SHEIKH PONDA NA VIONGOZI WA UAMSHO ALIPOWATEMBELEA GEREZANI

Sheikh Ponda Issa Ponda
 
Na Bakari Mwakangwale, An-Nuur — VIONGOZI wa Jumuiyaya UAMSHO Zanzibar wamesema kwamba pamoja na kuzuiwa kwao Gerezani, hawana shaka kuwa ipo siku hakiitasimama na hatimaye kupatikana Taifa Uhuru la Zanzibari.

Kauli hiyo wameitoa mbele ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi zaKiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, muda mfupi baada ya kukutanana viongozi hao Ijumaa ya wiki iliyopita katika Gereza la Kiinuamiguu, lililopo Mtaa wa Kilimani Zanzibar.

Sheikh Ponda, alifika gerezani hapo akiwa katika muendelezo wa ziara zake anazofanya nchini na kuongea na Waislamu, baada ya kumalizika kwa kesi yake na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje.

Akiongea na Mwandishi wa habari hizi katika ofisi za Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), Kinondoni, Jijini Dares Salaam, mapema wik ihii alisema alifanikiwa kuonana na viongozi wa UAMSHO na kuongea nao kwa muda wa dakika 45.

Alisema, Masheikh hao waliopo gerezani kwa muda wa miezi tisa sasa, wapo imara kiimani ambao walitumia fursa hiyo kumpa salamu kwa Wazanzibari huku naye akiwapa salamu kutoka kwa Waislamu wa Bara. “Hawana hofu pamoja na kushikili wa na Dola kwa muda wote huo, kwani wanachoamini wao kuwa wapo katika haki, na uimara wao unakuja kutokana na kuijua vizuri historia ya kupigania haki kuwa hata Mitume 
wa Mwenyezi Mungu, walipo tangaza haki, walipata misukosuko na kupigwa vita na watawala.” Alisema Shkh. Ponda, Akielezea hali za Viongozi hao wa UAMSHO.

Ponda, alisema kuwa Masheikh hao, MselemAli, Azan Khalid, Musa Juma pamoja nae Amir Farid Had, kwa kwa ujumla akiyatafakari maongezi yao anaona ni wazi kuwa msimamo wao ni kutorudi nyuma katika kupigania haki na zaidi alidai walimuambia hawana shaka kuwa ipo siku haki itasimama na batili itaondoka Visiwani humo. Alisema, Masheikh hao, walimtaka awafikishie ujumbe Wazanzibar katika mikutano yake kuwa wasiache kuzungumzia haki zao za msingi wanazodai kwani kwa kufanya hivyo ndiyo kuitendea haki Zanzibar.

“Katika fursa hii mliyoipata ya kuwahutubia Wazanzibar na hatimae Watanganyika, waambien imsimamo wetu bado ni uleule wa kutetea Taifa Uhuru la Zanzibari na bila shaka pia huo utakuwa ni Uhuru kwa Watanganyika pia,” alisema Sheikh Ponda, akimnukuu Amir Farid Had.

Sheikh Ponda alisema viongozi hao walimuagiza kutumia vema fursa ya mikutano yake Visiwani humo na hatimae Bara kwa kuinua hamasa za Waislamu huku wakimtaka kuwaelekeza kutumia vema mafunzo na misimamo waliyoitoa juu ya Taifa huru la Zanzibar.

“Darsa zetu bila shaka zimejenga imani na akida, vilevile zinatosha kuwa semina za kujitambua.

Lakini pia tulijenga hamasa kubwa na utayari wakutetea haki hadharani. Kama Waislamu hawatakiwi kurudi nyuma wasinyamaze hata kidogo”, alisema Sheikh Ponda, akidai kuwa huo ni ujumbe kutoka kwa Sheikh Mselem Ali.

Awali Sheikh Ponda, kwa upande wake aliwapa viongozi hao salamu na hisia za Waislamu wa Bara kufuatia ziara zake katika mikoa kadhaa ya Tanzania Bara zilizoandaliwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu mara baada ya kutoka Gerezani.

“Waislamu wa Bara wanatambua msimamo wenu wa kupigania haki, pia wanaamini kukamatwa kwenu ni ukweli wa methali isemayo ‘kiza kinapozidi kuwa kinene ndivyo kupambazuka kunavyokaribia’ hivyo wako pamoja nanyi.” Alisema SheikhPonda, akirejea kauli yake mbele ya viongozi wa UAMSHO Gerezani.

Katika ziara yake hiyo Visiwani humo, Sheikh Ponda, pia alipata fursa ya kuwahutubia maelfu ya Wazanzibar katika mihadhara sita iliyoandaliwa na Jumuiya ya UAMSHO katika maeneo mbalimbali ya Unguja.

Akiwahutubia maelfu ya waumini waliohudhuria katika muhadhara uliofanyika Mkoa wa Mjini Maghribi Masjid Sahaba Daraja Bovu, Sheikh Ponda, aliwataka Waislamu wa Zanzibar kuchukua hadhari ya njama zinazopikwa kuvunja udugu wao kwa lengo la kuwagawa. Kwa mujibu wa Sheikh Ponda, alisema maelfu ya Waislamu waliokutana katika Msikiti wa harakati maarufu kwa jina la Msikiti wa Mbuyuni, walisema wanatafakari hatma ya viongozi wao wanaoshikiliwa na Dola kwa zaidi ya miezi tisa sasa.

“Msimamo kama huo ulitolewa tena katika mkusanyiko mkubwa uliofanyika siku iliyofuata (Ijumaa iliyopita) mara tu baada swala ya Ijumaa katika Msikiti wa kwa Mpendae kwa Kificho.

Kuonesha hisia zenu kama hivi bila shaka mnajenga nguvu kubwa ya pamoja na wakati utakapofika watawatoa tu viongozi wenu”. Alisema Sheikh Ponda, akiwahutubia waumini wa Nungwi.

Aidha Shkh Ponda, aliwataka waumini wa Nungwi kujiimarisha kwa miradi ya maendeleo kwa kutumia vizuri hazina kubwa ya ardhi waliyonayo ambayo imekuwa ikivamiwa kwa kasi kubwa na wawekezaji wa mahoteli ya kitalii, ambao kwa asilimia tisini wanaharibu utamaduni wa Mzanzibar.

Sheikh Ponda, alisema Jumuiya ya UAMSHO, inatarajia kufanya muhadhara mkubwa siku ya Ijumaa katika Msikiti wa Mbuyuni, lengo likiwa ni kufanyama jumuisho ya mihadhara iliyofanyika akiwa hukowiki iliyopita.

--
Rejea ya habari: An-Nuur no. 1081


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU