Facebook Comments Box

Monday, July 29, 2013

NITAJIUZULU NIKIBAINIKA NAUZA MADAWA YA KULEVYA - IDD AZZAN

Picture: Idd AzzanIdd AzzanSiku chache baada ya jina lake kutajwa kwenye waraka unaodaiwa kuwa barua kutoka kwa mmoja wa Watanzania waliofungwa katika jela huko Hong Kong, Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan amezungumza na kusema kuwa yupo tayari kujiuzulu ubunge ikiwa itabainika anajihusisha biashara ya dawa za kulevya.

Idd Azzan amekaririwa katika habari iliyoandikwa na mwandishi Bakari Kimwanga, na kuchapoishwa kwenye gazeti la MTANZANIA jana akisema kuwa hatua ya kuhusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya ni kutotenda haki mbele ya jamii hasa wapiga kura wake na Taifa kwa ujumla. Akasema mtu aliyendika barua ya tuhuma dhidi yake amedhamiria kumshushia heshima na huenda ana jambo limejificha.

Alisema kutokana na hali hiyo, anashindwa kuchukua hatua yoyote ya kufanya zaidi ya kuliandikia barua Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi dhidi ya barua hiyo kuweza kubaini ukweli wa jambo hilo.

Ni kweli nimeiona hiyo barua katika mtandao, inayodaiwa imeandikwa na kijana ambaye amekamatwa Hong Kong nchini China. Lakini ninajiuliza kama kweli yeye ni raia mwema, katika hili kwa nini hakutaka kutaja jina lake kwenye barua hiyo?

Hata nilipoisoma nimebaini kuwa huyo mtu ametumika na huenda kabisa hayupo nje ya nchi, kwani 
katika maelezo yake anataja jina la Balozi Philip Marmo kuwa amemsaidia hali ya kuwa hivi karibuni Rais Kikwete alimteua Balozi mpya Abdulrahman Shimbo na Marmo kuwa Balozi wa Shirikisho la Ujerumani.

Kingine naona alijaribu kuandika uongo kuweza kuaminisha jamii, kwani hata hilo jila la balozi mwanzo limetajwa jina la Bernard na kukatwa kwa wino. Ninapenda kulieleza Taifa kuwa naomba vyombo vya usalama vifanye uchunguzi wa jambo hili na nikibainika ninauza dawa za kulevya nipo tayari kujiuzulu ubunge wangu.

Kubwa haki itendeke katika kufanya uchunguzi wa jambo hili, ila ni lazima jamii na Watanzania kwa ujumla tusikubali kwa makusudi watu waichafue nchi yetu kwa chuki na fitna tu.

Sijawahi kuuza dawa za kulevya na hata katika familia yangu hakuna mtu anayefanya biashara hiyo haramu. Kila mmoja anajua kuwa Idd nilikuwa Diwani wa Kata ya Magomeni, huku kazi yangu kubwa ikiwa ni biashara ya magari na daladala ambayo ninaendelea nayo hadi sasa mbali ya ubunge kama nilivyopewa heshima na wapiga kura wangu wa Kinondoni.
Alipoulizwa kuwa ni hatua gani ikibainika hakuna ukweli wa jambo hilo baada ya vyombo vya usalama kufanya uchunguzi, Azzan alisema: “Ni ngumu kusema hatua gani nitachukua ikibainika hakuna ukweli, lakini nataka kusema kama yule aliyeandika barua hii angetaja jina lake ni wazi baada ya uchunguzi ningeweza kuomba ushauri kwa mwanasheria wangu hatua za kuchukua, lakini kwa kuwa hakutaja jina ni ngumu kuweza kuamua.” 

Source: WAVUTI

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU