Facebook Comments Box

Tuesday, July 30, 2013

TAMASHA LA SIMBA LAPELEKWA MBELE: TP MAZEMBE HAWATAKUJA KUSHIRIKI TAMASHA HILO

TAMASHA la kuazimisha siku ya Simba SC linaweza kusogezwa mbele kwa simu mbili, kupisha sikukuu ya Eid El Fitri hivyo kufanyika Agosti 10, badala ya Agosti 8, kama ilivyo kawaida yake.
Aidha, mpango wa Simba SC kucheza na mabingwa wa Afrika mara nne, Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umeshindikana kutokana na timu hiyo ya Lubumbashi kutingwa na michuano ya Kombe la Shirikisho.
Kikosi cha simba kilichopita kikiwa na wachezaji wazuri kama Mrisho Ngassa, Juma Kaseja, Haruna Moshi na Mwinyi kazimoto


Na kwa sababu hiyo, timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, Dar es Salaam sasa itacheza na SC Villa ya Uganda katika tamasha hilo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba ilitumai kucheza na Mazembe yenye wachezaji wake wa zamani wawili, Mbwana Samatta na Patrick Ochan ambao iliwauzua klabu hiyo miaka miwili iliyopita, lakini ratiba ya michuano ya CAF imeharibu mambo. 
Katika maendeleo mengine, wachezaji wa Simba SC waliokuwa na kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wanatarajiwa kujiunga na wenzao kambini, Bamba Beach, Kigamboni kuanzia leo jioni.
Wachezaji waliokuwa Stars ni viungo Amri Kiemba na Haroun Chanongo. Kiemba alicheza dakika zote 90 na kufunga la Stars ikilala 3-1 Uwanja wa Mandela, Namboole na kutolewa jumla ya mabao 4-1, baada ya awali kufungwa 1-0 Dar es Salaam wiki mbili zilizopita, wakati Chanongo aliingia uwanjani dakika ya 78 kumpokea John Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC.

SOURSE: BIN ZUBEIRY

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU