Facebook Comments Box

Wednesday, July 3, 2013

MUHIMBILI KUTENGENEZA CHUO KINGINE CHA UDAKITARI

Picha onayoonesha mchoro wa jengo

Na: Belinda Kweka- MAELEZO
CHUO Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili(MUHAS)  kipo katika mpango wa kujenga chuo kipya kwa ajili ya ufanyaji mazoezi kwa wanafunzi.Ujenzi huo  unatarajiwa kuanza Agosti mwaka huu katika eneo la Mloganzila Kibamba  ambapo , ukimalizika  utachukua wanafunzi 15,000  watakaosoma  taaluma  mbalimbali za afya. Akizungumza  na
waandishi wa habari  leo kwenye   Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa  yanayoendelea katika viwanja  vya  Mwalimu  J. K Nyerere  jijini  Dares Salaam (sabasaba) ,Afisa Mipango Mkuu wa chuo hicho Ulimbaga Kijobile alisema  uamuzi  huo umetokana na ongezeko la wanafunzi ni wengi.
Alisema  eneo hilo   lita wezesha wanafunzi hao kupata sehemu  za kusomea kwa ufanisi  kama vile  ya maabara za kisasa, madarasa, na sehemu za ufanyaji mazoezi.

“Tumeamua kuanzisha mradi kwa kujenga chuo kipya kwa sababu MUHAS ina sehemu ndogo na hatuwezi kuipanua kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa chuo ili kuweza kutosha kwa wanafunzi” alisema Kajobile.
Aidha alisema wanafunzi hao , walikuwa wakipata tabu katika kufanya mazoezi ,hivyo hulazimika  kwenda  hospitali za Mwananyamala na Amana.“Muda mwingine tunatumia hospitali nyingine ili kupata sehemu ya kutosha lakini hospitali hii itakayojengwa itasaidia kuchukua wanafunzi wote ili kuweza kufanya mazoezi yao bila usumbufu” alisisitiza Ulimbaga.
Alisema  ujenzi wa  chuo hicho, kinakadiriwa kujengwa ndani ya mwaka mmoja,ambapo  wanafunzi wa muhula wa kwanza wa mwaka 2015 wanatarajiwa kuanza.
Aliongeza  kuwa kitatoa huduma za kiafya kama hospitali nyingine hivyo wananchi wa eneo hilo wanashauriwa kufika mara baada ya ufunguzi wa chuo hicho ili kupata matibabu mbalimbali.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU