Ambrose
amesomewa mashtaka 21 ya kuua na kujaribu kuua wakati wa uzinduzi wa
kanisa hilo ambao mgeni rasmi alikua Balozi wa Vatican nchini, Askofu
Mkuu, Fransisco Padilla ambaye alikuwa na mwenyeji wake Askofu Mkuu wa
Jimbo Kuu la Arusha, Josephat Lebulu.
Katika
hatua nyingine Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas amesema
kuwa watuhumiwa watatu raia wa United Arab Emirates (UAE) Abdul Aziz
Mubrak (30) ambaye ni mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato, Fouad Saleem
Ahmed Hareez Al Mahri (29), Saeed Abdulla Saad (28) ambaye ni askari
Polisi na raia mmoja wa Saudia Arabia, Al Mahri Saeed Mohseens (29) wamekutwa hawahusiki na tukio hilo na wamekabidhiwa kwenye idara ya uhamiaji mkoani Arusha ili kuangalia kama waliingia kihalali nchini.
Sabas amesema watuhumiwa wengine bado wanahojiwa kuona namna gani wanahusika na kitendo hicho cha kigaidi.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog