Facebook Comments Box

Monday, May 13, 2013

MSANII LADY JAY DEE APOKEA HATI YA MASHITAKA LEO

 

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee (Pichani) muda si mrefu amepokea hati yake ya mashtaka kutoka katika mahakama ya Kinondoni ambapo ameshtakiwa na Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds FM baada ya kuwa na kutofautiana kwa muda.
Jaydee ambaye alikuwa Baraza la Sanaa ambapo alikuwa akiongea katika jukwaa la wasanii, alipata ujumbe wa kuitwa mahakamani na alipofika alikabidhiwa hati hiyo ambayo mwenyewe alikataa kusema makosa aliyoorodheshewa, na kusema kwamba anataka kwanza awasiliane na mwanasheria wake.
Kikubwa ambacho aliweza kusema kwa waandishi waliokuwa wameongozana naye ni kwamba, kesi itaanza kuunguruma tar 27 mahakamani hapo.
Kati ya vielelezo alivyopewa na mahakama ambavyo alivionesha kwa baadhi ya waandishi ni pamoja na nakala za magazeti na nakala za Post za blog yake pamoja na tweets!



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU