Facebook Comments Box

Saturday, March 16, 2013

SUNDERLAND YA ENGLAND YAIPIGA CHINI SIMBA SPORTS CLUB


SUNDERLAND ya England imevunja uhusiano wake na Simba baada ya kutoridhishwa na baadhi ya mambo

Klabu hiyo ya England sasa inafikiria kufanya kazi na Yanga au Azam ili kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya kukuza fursa ya uwekezaji na kutoa msaada wa kiufundi kwa klabu moja kati ya hizo.

Habari za ndani zinasema kwamba Sunderland ilianza kuwasiliana na uongozi wa juu wa Simba lakini kukawa hakuna mrejesho wowote kutoka kwa viongozi wa klabu hiyo ya barabara ya Msimbazi.

Habari zinasema Sunderland walituma barua pepe tatu (email) kwa uongozi wa juu wa Simba lakini baada ya kuona hakuna majibu wakaandika ya mwisho kuwajulisha kwamba wamesitisha urafiki kwani hawawezi kufanya mambo ya kimagumashi.

Endapo dili ya Simba ingefanikiwa wangekuwa wakipata vifaa mbalimbali, pamoja na misaada ya kiufundi na fursa kadhaa kila mwaka.

Awali Simba ambayo iliasisiwa mwaka 1936 ilikuwa ikitumia jina la Sunderland kabla kubadili na kuanza kutumia hili la sasa tangu 1971.

Simba ilipanga kuanzia kutumia jezi za Sunderland msimu ujao ambazo zina maandishi ya 'Invest in Africa' ambayo huvaliwa pia na Sunderland ya England, lakini kutokana na dili hilo kufa, Simba wataendelea kuvaa jezi zao za Kiliamanjaro

Simba imekuwa katika hali ambayo watafsiri wa mambo wanasema ni mgogoro wa chini chini kwa kuwa baadhi ya viongozi wake wa juu mameanza kujiuzuru mmoja mmoja huku mwenyekiti wa kilabu hiyo Mh Aden Rage aking'ang'ania kubaki madarakani.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU