Hii ni hali ilivyo sasa barabara ya uhuru baada ya barabara kukarabatiwa upya na lami iliyokuwepo kuondolewa na kuwekwa mpya. Kabla ya hapo maji yalikuwa yakituama na kusababisha eneo hili la barabara kuwa na mabonde na madimbwi mengi wananchi walipoona inakarabatiwa wakadhani kampuni iliyopewa kazi hiyo itazingatia hilo na maji hayatatuama tena. Cha kushangaza kwa mvua hizi ndogo maji yametuama tena kwa maana rahisi kampuni imechakachua kazi hii. Angalia picha hapo chini
Ukifika Rozana tu unaliona hilo dimbwi |
Hili ni eneo la buguruni sokoni karibu na kituo cha polisi cha buguruni. Angalia maji hayo yalivyo tuama. Malaria haikubaliki? Kipindupindu je? |
Kampuni imeshamaliza kazi hapo na lami mpya imewekwa |
kwa mbaali unaliona dimbwi alilotengeneza bwana injinia |
Ukiangalia vizuri utaona gari linavyowamwagia maji wapita njia pamoja na nyanya na matunda yanayowekwa hapo chini. Tunaolala hoi tunakazi sana |
Matope yaliyocchanganyikana na uchafu wa sokoni buguruni. |
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog