Mamlaka
ya Bandari Tanzania (TPA) imeongeza ukusanyaji wa mapato katika bandari
ya Dar es Salaam kutoka shilingi bilioni 28 mwezi Novemba hadi shilingi
bilioni 50 (dola milioni 18 hadi dola milioni 31) katika mwezi wa
Disemba, kufuatia kusimamishwa kwa muda maofisa 16 wa bandari wanaotuhumiwa kwa mwenendo usiofaa.
Maofisa
hao wa bandari, wakiwemo wakurugenzi wa ngazi za juu, walisimamishwa kwa
muda mwezi Disemba baada ya Wizara ya Usafirishaji kuanzisha uchunguzi
wa ndani kwa lengo la kutoa mwitikio wa malalamiko ya wateja kuhusu
kucheleweshwa katika bandari hiyo, kwa mujibu wa Waziri wa Usafirishaji
Harrison Mwakyembe.
Maofisa wa bandari wengine wasiopungua sita.
Uchunguzi huo, ambao bado unaendelea, uligundua kuwa waajiriwa wa
bandari walibadilisha mwelekeo wa biashara kutoka katika bandari kwenda
kwa kampuni ndogo za usafirishaji na utoaji mizigo wanazomiliki,
ukiukaji wa moja kwa moja wa mkataba wao wa ajira.
"Wateja
wanakimbia bandari yetu kwa sababu ya ucheleshaji wa kukusudia
unaofanywa na waajiriwa wasio na maadili ambao wanaongeza gharama za
kufanya biashara," Mwakyembe aliiambia Sabahi. "Hii ni kinyume na
mikataba yao ya ajira na wana mgongano wa maslahi na mwajiri wao ambae ni Serikali."
Miongoni
mwa viongozi wa bandari wa ngazi ya juu waliosimamishwa ni Mkurugenzi
Mkuu wa TPA Ephraim Mgawe, Mkurugenzi wa Mipango Florence Nkya,
Mkurugenzi wa Uhandisi Bakari Kilo, Mkurugenzi wa Mifumo ya Utawala
Maimuna Mrisho, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Ayub
Kamili, Naibu Mkurugenzi Mkuu Hamad Koshyuma, Naibu Mkurugenzi Mkuu
Julius Fuko, na Meneja wa Bandari Cassian Ng'amilo.
Mashtaka
rasmi bado hayajatolewa dhidi ya viongozi waliosimamishwa na bado
hawajajibu tuhuma zozote hadharani. Mwakyembe alisema Bodi ya
Wakurugenzi ya TPA itakutana hivi karibuni kutoa uamuzi wa mwisho
kuhusiana na ajira yao.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog