Facebook Comments Box

Friday, January 4, 2013

SAFARI YA YANGA YA MWAKA 1973 KUZINDUA TOTO AFRICA FC MWANZA (Part I)

Hii safari ilishirikisha vijana yaani Yanga B wakati huo ikiwa maarufu kama Yanga kids ila kwenye makala hii nitakuwa nikiita Yanga B haitakuwa vizuri kuielezea safari bila kujua timu ya Yanga B ilipatikanaje. Mwaka 1972 Yanga iliajiri kocha kutoka Romania ambaye alikuwa akiitwa Victor Stanculescu. Kama walivyo wazungu wengi na kanuni ya mpira inavyohitaji timu kuwa na timu ya vijana ambao ndio wajenzi wa timu kubwa ijayo. Kocha Victor ambae baadae alikuja kuwa Profesa alichagua vijana 44 ambao alifanya nao mazoezi na mwaka 1973 akawa tayari na vijana wake 22 ambao ndio aliokuwa akiwahitaji katika Yanga B. hakuwacha wale 22 wengine hivihivi aliwaweka katika makundi mawili ya wachezaji 11 kila kundi akalipa mipira 5 na kuwaambia wakaunde timu zao sehemu nyingine. Enzi hizo Yanga wakiwa wamejipanga vilivyo kwa zamani Yanga ikijulikana kama Serikali kulikuwa na stoo kama 5 ambazo za vifaa stoo namba 1 ilikuwa na mipira imejaa namba 2 ilikuwa na viatu namba 3 ilikuwa na mabegi namba 4 ilikuwa na jezi na namba tano ilikuwa na soksi na stoo zote zilikuwa zimejaa. Kipindi hicho mwenyekiti wa Yanga alikuwa mzee Mangara.
Waliosimama kuanzia kulia Mzee Kwala, Sululu, Chotta, Muhamed Mkweche, Muhamed Yahaya "Tostao" (anaechungulia jina lake halijapatikana) Kassim Manara,Shirsaz Shariff (wawili wa mwisho majina yao hayajapatikana) Waliochuchumaa kuanzia kushoto Abdulrahman, kibonge, Bilal Kabange, Muhamed Rishard Adolph, Muhamed Sengendo, Gordian Mapango, Jaffar Abdulrahman (wawili waliobaki majina yao hayajapatiakana ila kati ya hao wote ambao majina yao hayajapatikana mmoja wao ni Dr Ramadhan Dau)
Wachezaji wa Yanga B walikuwa wakipewa maziwa kila mtu mara mbili kwa wiki japo mhasibu wa Yanga alikuwa mgumu kuna siku profesa Victor alikuwa akichukua kofia ya mzee Mangara na kuitembeza kwa washabiki waliokuja kuangalia mazoezi ili wachangie hela kwa ajili ya maziwa ya Yanga B. Hili lilikuwa halimpendezi sana Mzee Mangara na akamuamrisha mhasibu awe anatoa hela ya maziwa ya Yanga B kila inapo hitajika.
Wakati wa mwanzo ilikuwa shida sana kwa Profesa Victor kuwasiliana na wachezaji kwa kuwa wengi walikuwa hawajui kingereza ndipo alipo mfuata Sunday Manara kumueleza tatizo hilo. Sunday Manara akamchukua Profesa hadi Civil Service Training Centre kurasini wing  ambapo kwasasa ianjulikana kama Tanzania Institute of Account (TIA) ambapo alimkutanisha na Mzee Bilal Kabange ambae alikuwa kipa wa chuo. Profesa Victor alifurahi sana kwa kuwa alikuwa akitafuta kipa na Bilal Kabange alikuwa kipa ambae angemfaa kwa kiwango cha juu na juu ya yote alikuwa anaongea kiingereza vizuri kuliko hata yeye Profesa Victor maana yeye alikuwa ni Mromania.
Mwaka 1973 Yanga ikapewa mwaliko wa kuenda kufungua tawi la Toto africa Fc ya Mwanza ( Itaendelea Ijumaa Ijayo Mambo ya Kassim Manara na Adolph Rishard)


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU