Facebook Comments Box

Friday, January 4, 2013

AIR TANZANIA YAANZA SAFARI ZA KIGOMA

Mkurugenzi wa ATCL Kapteni mstaafu Lazaro

Air Tanzania (ATCL) kuanza safari za kigoma Alhamisi ya tarehe 10/01/2013. Akizungumza na blog hii mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Kapteni Msataafu Milton Lazaro amesema safari hizo zinaanza baada ya uwanja wa ndege wa kigoma kumalizika ujenzi wake. Ndege hiyo itakuwa ikibeba abiria hamsini kutoka Dar es Salaam mpaka kigoma.
Aliongeza vilevile kuwa wanasubiri kukamilika kwa viwanja vya ndege vya Tabora na Mpanda ili waanze kurusha ndege zao katika anga za mikoa hiyo na kutoa huduma murua kwa wakazi wa mikoa hiyo.
Vilevile ATCL itaanza safari za Mbeya na baadae kuzindua safari za Arusha kwa kupitia Zanzibar. Akiongea kwa kujiamini anasema kuwa kabla ya mwaka huu kuisha watakuwa wameongeza ndege tatu zaidi.

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU