Facebook Comments Box

Sunday, January 20, 2013

ANGALIA PICHA ZA MAANDALIZI YA KUAPISHWA RAIS OBAMA WA MAREKANI


Maandalizi makubwa yafanyika jijini Washington DC kwa Sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Marekani Barack Obama yameanza kukamilika.

Vyombo vya Habari mbali mbali hapa nchini Marekani vimekuwa katika kukamilisha matayarisho ya kupata matukio ya kuapishwa Rais Barak Obama kwa muhula wa Pili Ikiwa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Kiafrika kuchaguliwa kwa mara ya pili na hivyo kuifanya sherehe hiyo kuwa ya Kihistoria.

Sherehe hizo zitafanyika katika viwanja vya National Mall na Memorial Parks zitahudhuriwa na mamilioni ya Raia wa marekani na wageni kutoka nchi mbali mbali kote ulimwenguni.

Rais Obama wa Marekani alichaguliwa kwa kura nyingi baada ya kumshinda mgombea wa kiti cha chama cha Republican Mitt Romney na kuingia awamu ya pili ya Urais ya Urais wa Marekani

Karibia mwenzi mzima ufundi wa maandalizi ya Obama inauguration 2013 yaliokua yakifanyika katika maeneo mbali mbali ya Jijini Washington DC yaaza kutia Sura, hapa ni Jengo la Congress ya Marekani Jijini Washington DC.
Baadhi ya ufundi uliokamilika katika jingo la Capitol Hill liliopo washington DC na viti vilivyopangwa rasmi kwa ajili ya wageni wanunuzi watikiti za 2013 Inauguration History ndio makazi yao yatakapokua hapa kwa siku ya Jumatatu Jan. 21, 2013 
Cheif wa swahilivilla blog Abou Shatry akipata picha ya 2013 katika jingo la Congress ya Marekani liliopo washington DC katika jingo la Capitol Hill liliopo down town Washington DC Nchini Marekani.
Picha 2008 Inauguration History: Hivi ndivyo itakavyokua Siku ya Jumatatu Januwari 21, 2012 kwenye Jumba la Congress ya MarekaniDown Town Washington DC.
Sehemu kubwa ya sherehe ya kuapishwa kwa rais Obama ikifanyiwa ukarabati wamuda.
Rubber floor tiles zikitandazwa maeneo ya sakafu zilizokua na mchanga kwaajili ya kuhifadhi tope tope zisitimke na kuharibu eneo hilo kubwa la National Mall,
Kukanyaga mchanga Marekani ni kosa kubwa na ndio maana wameweka Rubber floor tiles kwaajili ya kukanyagia ili kunusuru michimbuko ya tope tope na kutoshafua barabara kwa msongamano wa watu watakaomiminika kutoka Nchi mbali mbali kuja kushuhudia kuapishwa kwa Obama
Sehemu iliotandikwa Rubber floor tiles: Hivi ndivyo Rubber floor tiles zinavyotandikwa kwenye michanga ili kunusuru topetote raia wasichafuwe maeneo ambayo bado yanafanyiwa ukarabati sehemu ya National Mall Jijini hapa.
Hivi ni baadhi ya yyoo vya Potty shortage vinavyotumika kwa haja ndogo na kubwa viko tayari kwaajili ya raia na wa geni watakao miminika kuanzia kesho Jumapili na Jumatatu siku ya Obama's inauguration
Fundi mitambo wa NBC NEWS akianda mpango mzima wa kuahabarisha sherehe za kuapishwa kwa rais wa Marekani Barack Obama Live
Banda la CBS NEWS lilijengwa kwa muda vile vile wako tayari kwa kutoa huduma za kuhabarisha matangazo ya moja kwa moja kwenye kumbukumbu za 2013 Inauguration
Channel marufu ya CNN wakia kwenye uwanja wa National Mall na wao pia wapo tayari kwa kutoa huduma za kuhabarisha na matangazo ya moja kwa moja kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Obama 2013 Inauguration 
Basi lililowakilisha baadhi ya wafanyakazi wa CNN kumbukumbu ya 2013 Inauguration ndani ya Jiji la Washington DC 
Basi jengine lililowakilisha wafanyakazi wa C-SPAN kumbukumbu ya 2013 Inauguration ndani ya Jiji la Washington DC 
Kamera iliopo mbele ya Presidential Inaugural Review Stands, in front White House Washington, D.C. baada ya kuapishwa kwa Obama. hii ni moja itakayo tumika kwenye Inaugural Review Stands
Cheif wa swahilivilla akia mbele ya White House na mmoja wa wafanya kazi wa Super Control Camera ambayo kwa jina wanaita Gym Camera inauwezo wa kunyanyuka juu umbali wa futi 16 na kuhabarisha Live.
Sony Camera ipo tayari kwa kuhabarisha mbele ya Presidential Inaugural Review Stands, mbele ya White House Jijini Washington DC.
Nyuma ya Presidential Inaugural Review Stands ni White House kuna ujia mrefu wa Red carpet ndio atakaotumia kuingilia kwenye Review Stands.
Cheif wa swahilivilla blog Abou Shatry akiwa mbele ya Presidential Inaugural Review Stands ambayo kutumika kwa ajili ya uzinduzi wa Rais Barack Obama baada ya kuapishwa.
Mjengo wa Matangazo pamoja na Camera LIVE uliojengwa kwa moda mbele ya White House
Benchi nyingi zilizojengwa kwa ahili ya wageni na rais kutoka sehemu mbali mbali watatumia kukalia wakati wa Parade


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU