Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’,
Charles Boniface Mkwasa, ametangaza wachezaji 20 watakaounda kikosi
kitakachosafiri mwishoni mwa mwezi huu kwenda Nigeria kwa ajili ya
mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya Taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.
Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa
kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini
utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G
ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo
iliyojitoa katikati ya mashindano.
“Tanzania hatuwezi kuupuuza mchezo huu, tunaupa umakini kabisa kwa sababu tunacheza ugenini ambako matokeo mazuri
yanaweza kutusongesha mbele na kuingia ndani ya timu 99 bora katika
viwango vya FIFA,” amesema Mkwasa.
Katika kikosi chake, Mkwasa ametangaza kutomjumuisha Mshambuliaji wa
Kimataifa, Thomas Ulimwengu anayecheza klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutokana na majeruhi ya paja kama ilivyo
kwa Juma Abdul wa Young Africans ambaye aliumia katika mchezo wa kuwania
Kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.
“Timu ilitarajiwa kuingia kambini Agosti 28 siku ya Jumapili, mchezo huo ni wa kukamilisha ratiba ambapo Misri tayari
wameshafuzu fainali za Afrika,” alisema Mkwasa na kuongeza kuwa kuna
mchezaji wa Tanzania, Said Carte Mhando anamfuatilia ili ikiwezekana
baadaye amwite kuchezea timu ya Taifa. Anachezea Klabu ya Brencia Calcio
ya Italia.
Wachezaji walioitwa:
Makipa; Deogratius Munishi (Young Africans) na Aishi Manula (Azam FC)
Mabeki
Kelvin Yondani (Young Africans),Vicent Andrew (Young Africans)
Mwinyi Haji (Young Africans),Mohamed Hussein (Simba SC)
Shomari Kapombe (Azam FC) na David Mwantika (Azam FC)
Viungo
Himid Mao (Azam FC),Shiza Kichuya (Simba SC),Ibrahim Jeba (Mtibwa Sugar),Jonas Mkude (Simba SC),Muzamiru Yassin (Simba SC),Juma Mahadhi (Young Africans) na Farid Mussa (Tenerif ya Hispania)
Washambuliaji
Simon Msuva (Young Africans),Jamal Mnyate (Simba SC),Ibrahim Ajib (Simba SC),John Bocco (Azam FC) na Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog