Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umeamua kuongeza safari ya tatu ya treni ya abiria ya kawaida kwenda bara ambayo itaondoka Dar es Salaam kila Jumapili, safari ya kwanzai takuwa Jumapili hii ya Septemba 04,2016 saa 9 alasiri.
Taarifa imeainisha kuwa treni hiyo ya huduma ya kawaida itakuwa na mabehewa 12 kutokea Dar es Salaam ikiwa na mabehewa manane ya daraja la 3, mawili daraja la pili kulala na mawili daraja la kwanza. Katika stesheni za Morogoro na Dodoma yataongezwa mabehewa mawili mawili ya daraja la tatu.
Aidha treni ya Deluxe imebadilishwa siku ya kuondoka badala ya Jumapili kwa sasa kuanzia Septemba Mosi, 2016 itakuwa inaondoka siku ya Alhamis saa 2 asubuhi kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam.
Halikadhalika mabadiliko haya pia yataongeza safari za treni ya kwenda Mpanda kutoka Tabora badala ya 2 za sasa zitakuwa 3
kwa wiki ambazo ni Jumatatu, Jumatano na Jumamosi..
Wakati huohuo Uongozi wa TRL umefanya uamuzi wa kihistoria
wa kupeleka huduma za kuuzwa tiketi za safari zake mjini Kasulu ambapo kuanzia Septemba mosi itafungua kituo cha Reli ambacho kitafanya kazi ya kutoa huduma hiyo kwa wasafari wanaotoka Kasulu mjini na maeneo ya jirani .
Kwa uamuzi huo TRL imetoa nafasi za tiketi za behewa moja la daraja la 3. Pia kuna mpango wa kufungua kituo kama hicho siku zijazo mjini Kibondo hali itakaporuhusu kulingana na mahitaji halisi ya abiria.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Nd Focus Makoye Sahani,
Dar es Salaam,
Agosti 23, 2016.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Nd Focus Makoye Sahani,
Dar es Salaam,
Agosti 23, 2016.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog