Facebook Comments Box

Friday, November 27, 2015

MSHAURI WA RAISI WA BURUNDI ANUSURIKA KIFO

Mshauri wa Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amenusurika shambulio alipokuwa akitoka nyumbani kwake katika eneo la Kajaga, magharibi mwa mji mkuu Bujumbura.
Zenon Ndaruvukanye alinusurika bila majeraha yoyote, lakini mlinzi wake, ambaye alikuwa afisa wa polisi, alifariki kutokana na majeraha ya risasi.
Washambulijai walitoroka wakitumia gari aina ya Toyota  Hilux lakini polisi walipashana habari na gari lao likazuiwa maili kadha kutoka Kajaga. Waliacha gari hilo na kutorokea soko lililo karibu, lakini mwishowe wawili walikamatwa. Mmoja wao alifanikiwa kutoroka.

Gari hilo aina ya Toyota Hilux lilipatikana na silaha mbalimbali zikiwemo bunduki aina ya AK47 na guruneti. 
Polisi baadaye walipelekwa kwenye nyumba moja viungani mwa mji wa Bujumbura ambapo walipata silaha zaidi.
Mji wa Bujumbura umekumbwa na machafuko ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 200 tangu Aprili.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU