Facebook Comments Box

Tuesday, October 28, 2014

AJALI KONA YA JETI: LORI LAIANGUKIA HIACE


Kumetokea ajali mbaya mida hii maeneo ya Jeti Lumo mwisho wa lami ambapo gari kubwa la mizigo limeangua daladala iliyokuwa kituoni.


Ajali hiyo imetokea wakati gari hilo semi-trailer ikikata kona pale mwisho wa lami ambapo kontena lilianguka na kutua juu ya bodi ya daladala.


Mtoa taarifa wangu amesema hali ni mbaya na bado hajajua idadi ya vifo na majeruhi ujumla.Pia gari imepondeka sana jambo ambalo linaashiria hatari zaidi.


Kuna gari la kunyanyua makontena limeshafika pale lakini limeshindwa kutoa msaada wa uhakika kutokana na kuzidiwa uzito na kontena ambapo likijaribu kunyanyua kontena ushuka.

Hamna mtu yoyote aliepoteza maisha maana Hiace hiyo ilikuwa imepaki kusubiri muda wake wa kupakia abiria.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU