Facebook Comments Box

Tuesday, September 23, 2014

IKIFIKA MACHI GHARAMA YA KUUNGANISHA UMEME NYUMBANI ITAKUWA BURE

Gharama za kuunganisha umeme wa majumbani zitatolewa bure kuanzia mwezi Machi mwakani baada ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, kukamilika kwa asilimia 90.

Aidha gharama za matumizi ya umeme wa majumbani na viwandani zitapungua kwa kiasi kikubwa baada ya mtambo huo kuanza kufanyakazi.

Msemaji Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, alisema hayo jana alipotembelea mtambo huo Kinyerezi akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa na Waandishi wa habari.

Alisema kuwa gharama za watumiaji wa umeme kwa Tanzania ziko chini kwa asilimia tano ukilinganisha na nchi za Uganda (asilimia 24) na Burundi (asilimia 20).
“Mtambo wa kusafirishia umeme wa gesi ambao ukubwa wake ni kama ule wa Ubungo umekamilika kwa asilimia 90.

Alisema kuwa serikali imeajiri wafanyakazi Watanzania kwa asilimia 95, na ifikapo Januari vijana 60, watapelekwa nchini China kwa masomo ili wapate ujuzi wakuendesha mitambo hiyo.

Mhandisi anayesimamia mradi huo, Saimoni Gilma, alisema mradi huo umetumia Dola za Marekani milioni 103, ambazo zote zimelipwa na Serikali ya Tanzania.
Alisema ujenzi wa miundombinu ya mitambo hiyo umekamilika kinachosubiriwa ni kuletwa kwa mitambo hiyo kutoka bandarini.

Aidha, nyumba za wafanyakazi, watakaoendesha mitambo hiyo zimekamilika kwa ajili ya kuanza kazi. Alifafanua kuwa mabomba ya gesi yaliotandazwa aridhini kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ni transfoma 200. Na yatawekewa ulinzi mkali ikiwa ni pamoja na ulinzi wa helikopta itakayokuwa inazunguka usiku na mchana.

Alisema kuwa gharama za kuweka umeme majumbani zitagharamiwa na nchi ya Japan na Finland, wananchi watatakiwa kutoa sehemu ya viwanja vyao au mashamba ili kupisha bomba hilo kupita.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU